Profesa Muhongo: Tuna nishati ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema Tanzania kwa sasa ina hazina ya kutosha ya makaa ya mawe na gesi itakayowawezesha wawekezaji kupata nishati ya uhakika.

Waziri Muhongo pia ameahidi kuendeleza mradi wa usambazaji umeme vijijini ili kutimiza lengo la kila mtanzania kuwa na uhakika wa kupata nishati ya umeme.

Profesa Muhongo amesema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kikanda wa masuala ya nishati endelevu uliwakutanisha washiriki kutoka nchi kadhaa ndani na nje ya bara la Afrika.

Katika mkutano huo, Waziri Muhongo aliwataka wadau hao kutafuta suluhisho la upungufu wa nishati kwa kuzingatia malengo ya milenia yanayotaja nishati kama moja ya sababu za kuinua uchumi.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez alisema nchi za Afrika zinahitaji kutumia teknolojia, sera na uwezo walio nao katika kupambana na suala la upungufu wa nishati huku umoja huo ukiahidi kutumia jumla ya dola za Kimarekani bilioni mbili katika kuwezesha upatikanaji wa nishati endelevu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post