Picha: MWILI WA MPIGA PICHA MAARUFU MPOKI BUKUKU WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Nape Nnauye ameongoza wakazi wa jiji la Dar es salaam kuaga mwili wa mpiga picha Mwandamizi wa Magazeti ya The Guardian Limited yanayochapisha magazeti ya Nipashe, The Guardian, Mpoki Bukuku (44) aliyefariki dunia ijumaa iliyopita saa chache baada ya kugongwa na gari katika eneo la ITV jijini Dar es salaam wakati akitka kazini.


Wengine waliomuaga marehemu Mpoki ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni  Freeman Mbowe na mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea aliyewakilisha Chama Cha Wamiliki wa vyombo vya habari (Moat).

Akizungumza,Nape alisema tasnia ya habari imepoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa kwa taifa kupitia taaluma ya habari huku akiwataka wana habari kuiga kazi nzuri zilizofanywa na Mpoki Bukuku wakati wa uhai wake.

Naye Mbowe alimuelezea Bukuku kama mpambanaji aliyefanya kazi yake kwa weledi.

Msemaji wa familia, ambaye ni kaka wa marehemu, Gwamaka Bukuku, amewashukuru watu wote kwa kujitokeza ambapo amewaomba kuendeleza umoja wao kama walivyouonyesha katika msiba huo.

“Mwili wa marehemu baada ya kutoka hapa utasafirishwa kwenda mkoani  Dodoma nyumbani kwa wazazi wake kwa ajili ya mazishi kesho Jumanne Desemba 27,2016 ”amesema.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Mpoki Bukuku
Mheshimiwa Nape Nnauye akiteta jambo na Mheshimiwa Freeman Mbowe

Mheshimiwa Freeman Mbowe akiaga mwili wa marehemu Mpoki Bukuku- Picha zote kwa hisani ya Mo blog

TAZAMA PICHA ZAIDI <<HAPA>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527