HII NDIYO MIKOA NANE INAYOONGOZA TANZANIA KWA KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU


Kituo cha Sheria na Haki za BInadamu (LHRC) kimetoa Ripoti ya Mtazamo wa Hali ya Kisiasa Tanzania kwa mwaka 2016 ambayo miongoni mwa mambo mengi yaliyoonyeshwa katika ripo hiyo ni pamoja na mikoa iliyokumbwa na matukio mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
 
Hapa chini ni orodha ya mikoa yenye hatari kwa wakazi wake kutokana na kukiuka haki za binadamu.

Simiyu na Kaskazini Unguja:

Mikoa hii miwili kwa mwaka 2016 imekumbwa na changamoto kubwa katika uhuru wa kujieleza, uhuru wa kukusanyika na haki ya kupiga kura. Lakini kwa upande mwingine mikoa hii imepata alama za juu zaidi katika matokeo ya mtazamo kuhusu haki za kiraia na kisiasa, hasa kwa upande wa haki ya kuishi.

Songwe, Tabora na Shinyanga:

Mikoa hii ilipata alama za chini zaidi ukilinganisha na mikoa mingine yote. Mikoa yote ilikuwa na alama za chini sana kwenye uhuru ya Kukusanyika na haki ya kuishi-mauaji na ukatili mikononi mwa vyombo vya dola. Kama serikali za mikoa zitaendelea kuminya uhuru wa kukusanyika, kushughulikia mauaji yanayotokana na imani za kishirikina na matukio ya kujichukulia sheria mikononi, basi itakua ngumu kupata mwenendo chanya katika mikoa hii.

Morogoro, Arusha na Manyara:

Katika mikoa hii kuna ongezeko kubwa la migogoro ya ardhi ambayo inaweza kupelekea watu kujichukulia sheria mkononi au mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola. Migogoro hii hasa husababishwa na mvutano kati ya wakulima na wafugaji ambapo mara nyingi hupelekea vifo vya raia.
Mbali na mokoa hayo, kituo cha haki za binadamu pia kilitaja haki za raia zilizoongozwa kukiukwa kwa mwaka 2016 ambazo ni pamoja na;

Haki ya Kuishi-Kujichukulia Sheria Mkononi:

Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro, ambayo kwa sehemu kubwa ni mijini, iliongoza kwa kiasi kikubwa kwenye ukiukwaji wa haki hii. Kuna haja ya polisi na viongozi kurudisha imani ya wananchi juu yao ili kupunguza matuko ya kujichukulia sheria mkononi.

Uhuru wa Kutoa Maoni:

Athari ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari zitakuwa ni za muhimu sana kufanyiwa uchambuzi kwa mwaka 2017 hasa kwa kuwa uhuru wa vyombo vya habari umeelezwa kuwa miongoni mwa matatizo katika mikoa iliyopata alama za chini. 

Ukizingatia shinikizo ndani nan je ya nchi, itakuwa muhimu kuangalia kama Serikali itayafanyia kazi mapendekezo ya watetezi wa haki za 21 Matukio Makubwa yaliyotokea Mwaka 2016 Mtazamo wa Haki za Kiraia na Kisiasa 2016 Mikoa na Haki za Kuangalia mwaka 2017 Methodologia na Alama binadamu ya kurekebisha vipengele vya sheria hiyo vinavyominya haki.

Uhuru wa Kukusanyika:

Tumeshuhudia zuio la mikutano na mikusanyiko ya kisiasa kwa mwaka 2016, kitendo ambacho kimepelekea mtazamo kwamba uhuru wa kukusanyika imeminywa. Japokuwa Jeshi la Polisi baadae liliondoa zuio hilo, kitendo hicho kiliendelea kuathiri mtazamo kuhusu uhuru wa kukusanyika.

Haki ya Kuishi – Mauaji na Ukatili Mikononi mwa na Vyombo vya Dola:

Matukio ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola yamechangia kwa kiasi kikubwa kushusha alama za haki katika mikoa mingi. 

Japokuwa kumekuwa na ongezeko la mashtaka ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola, ikiwemo askari polisi wawili kukutwa na hatia ya mauaji hivi karibuni, kauli na matamko mbalimbali za viongozi wa serikali ambayo yanaweza kuchochea mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola yanaweza kuwa chanzo cha mauaji pia.
Unaweza kupakua ripoti nzima hapa chini;
 
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post