AJALI YA GARI DOGO NA HIACE YAUA WATU 9 IRINGA

Watu tisa wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Ifunda mkoani Iringa jana baada ya lori kugonga gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace. 


Inaelezwa kuwa dereva wa lori hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, alishindwa kufunga breki na kuigonga Hiace hiyo iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara. 

“Lori limeharibika kabisa na Hiace pia imeharibika kabisa,” wanaeleza mashuhuda.

“Lori hilo liliposhindwa kufunga breki liliigonga Hiace ambalo lilikuwa na abiria na kwenda mbele na kisha kugonga watembea kwa miguu,,” 

 Inaelezwa kuwa ajali hiyo iliyotokea jana jioni, madereva wa magari hayo wote wamejeruhiwa na wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa pamoja na majeruhi wengine. 

“Dereva mmoja yupo chumba cha upasuaji kwa kuwa mguu wake umevunjika na mwingine yupo wodini,” .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post