Picha 65: MAHAFALI YA 8 KIDATO CHA NNE MWAKA 2016 KOM SEKONDARI SHINYANGA MJINI


Jumamosi,Novemba 12,2016- Hapa ni katika shule ya Sekondari KOM (Kom Sekondari) iliyopo eneo la Butengwa mjini Shinyanga,barabara ya kuelekea Old Shinyanga ambako leo kumefanyika mahafali ya 8 ya shule hiyo.



Jumla ya wanafunzi 144 wamehitimu kidato cha nne mwaka 2016.


Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wazazi na walezi wa wanafunzi hao alikuwa Afisa Elimu wa mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi.



Shule ya sekondari Kom ilisajiliwa mwaka 2006 ikiwa na kauli mbiu ya "Elimu Bora Kwa Wote" mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi 540.


Shule hiyo ambayo imejizolea umaarufu mzuri wa kitaaluma ina majengo ya madarasa 16,walimu 27,maktaba moja,maabara mbili za sayansi,chumba cha kompyuta,za walimu,umeme wa TANESCO,maji kutoka ziwa Victoria,mwaka 2017 inarajia kuanzisha kidato cha tano na sita na tayari kuna bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha 65 za matukio yaliyojiri wakati wa mahafali hayo..Tazama hapa chini
Awali,Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akitembelea maonesho ya kitaaluma katika jengo ambalo linatarajiwa kuwa bweni la wanafunzi wa kike baada ya shule ya sekondari Kom kuanzisha darasa la Kidato cha tano mwaka 2017.Pichani kulia ni wanafunzi wa Kom sekondari wakimwonesha kwa vitendo mgeni rasmi masomo yao
Maonesho ya taaluma yakiendelea
Mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi( wa tatu kutoka kushoto) akiwa nje ya jengo la bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Kom
Kulia ni mkurugenzi wa Kom sekondari Jackton Koyi akiongoza na mgeni rasmi,afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi baada ya kutembelea maonesho ya taaluma
Mgeni rasmi,Mohammed Kahundi na viongozi mbalimbali wa shule ya sekondari Kom wakiwa katika shule hiyo
Mgeni rasmi Mohammed Kahundi (kulia mbele)akiwa na wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kom wakati wa maandamano ya wahitimu hao kuelekea ukumbini.Nyuma yake ni mkurugenzi wa Kom Sekondari Jackton Koyi,wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Peter Kuguru
Mgeni rasmi Mohammed Kahundi ambaye ni afisa elimu mkoa wa Shinyanga akikata utepe wakati wa mahafali ya 8 ya kidato cha nne Kom shule ya sekondari Kom
Mgeni rasmi Mohammed Kahundi ambaye ni afisa elimu mkoa wa Shinyanga baada ya kukata utepe
Wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2016 shule ya sekondari Kom wakiingia ukumbini kwa madaha
Wahitimu wakiingia ukumbini
Meza kuu wakipokea maandamano ya wahitimu: Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa shule ya Kom sekondari Mwita Waryoba,akifuatiwa na mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Peter Kuguru,mgeni rasmi Mohammed Kuguru,mkurugenzi wa shule ya sekondari Kom Jackton Koyi na meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui
Wahitimu wakiingia ukumbini
Wahitimu kidato cha nne Kom sekondari mwaka 2016 wakisalimia wazazi na walezi waliohudhuria mahafali hayo ya 8
Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Wahitimu wakitoa burudani kwa kucheza
Wahitimu wakitoa burudani


Wazazi wakiwa eneo la tukio


Mkuu wa shule ya sekondari Kom Mwita Waryoba akizungumza wakati wa mahafali hayo ambapo alisema dira ya Kom sekondari ni kutoa elimu bora kwa kila mwanafunzi ndiyo maana wamekuwa wakifanya vizuri katika mitihani yote ya kitaifa.Alisema mwaka 2015 wanafunzi waliohitimu kidato cha nne ni 160 kati yao 142 walijiunga kidato cha tano.


Wazazi wakiwa wamekaa
Mahafali yanaendelea,wazazi wakijipiga picha
Keki maalum kwa ajili ya mahafali ya 8 ya shule ya sekondari Kom
Wahitimu kidato cha nne 2016 Kom sekondari wakikata keki
Zoezi la kukata keki linaendelea
Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kom wakimlisha keki mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi
Wahitimu wa kidato cha nne 2016 wakimlisha keki mwenyekiti wa bodi ya shule Peter Kuguru
Wahitimu wakimlisha keki mkurugenzi wa Kom sekondari Jackton Koyi
Mkurugenzi wa Kom sekondari Jackton Koyi na mmliki wa Kom sekondari Magreth Koyi wakifurahia jambo
Wahitimu wa masomo ya kidato cha nne shule ya sekondari Kom wakiimba wimbo wa shule yao
Wahitimu wa kidato cha nne Kom sekondari wakiwa wamekaa
Wahitimu wa kidato cha nne Kom sekondari 2016 wakitafakari
Wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2016 Kom sekondari wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa mahafali yao
Wazazi wakiwa eneo la tukio
Mhitimu wa kidato cha nne 2016 Kom Sekondari Ruth Elias akisoma risala ambapo alisema walianza kidato cha kwanza wakiwa wanafunzi 109 na wamemaliza masomo ya kidato cha nne 2016 wakiwa 144 kati yao wanafunzi wa kike ni 60 wa kiume 84
Wazazi wakifuatilia risala ya wanafunzi: Katika risala yao wanafunzi hao walizitaja changamoto zilizopo shuleni hapo kuwa ni wanafunzi kuchelewa kufika shuleni pindi shule inafunguliwa sambamba na wazazi kuchelewa kulipa ada hivyo walitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi kubadilika na kuwahamasisha watoto wao kufika shuleni mapema na kuwalipia ada kwa wakati
Burudani ikachukua nafasi yake: Kundi la vijana maarufu kwa jina la Young Sungusungu wakicheza 
Mkurugenzi wa Kom Sekondari, Jackton Koyi akitoa neno wakati wa mahafali hayo ambapo alisema shule hiyo hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 540,walimu 27 na mazingira rafiki ya kujifunzia kwa wanafunzi hali inayofanya shule hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.Alisema mahafali hayo yanaenda sambamba na kuadhimisha miaka 11 tangu kuanzishwa kwa shule
Mkurugenzi wa Kom Sekondari Jackton Koyi alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto ya gharama za kuendesha shule alieleza kuwa mwaka 2017 wataanzisha kidato cha tano na sita na tayari wa shule ya awali na msingi
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kom wakionesha mchezo wa sarakasi
Vijana wakionesha mchezo wa sarakasi
Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Kom Peter Kuguru akizungumza wakati wa mahafali hayo ambapo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wazazi kuwalipia ada kwa wakati watoto wao
Wanafunzi wa Kom sekondari wakionesha mchezo wa igizo
Igizo linaendelea
Vijana wakitoa burudani
Wageni waalikwa wakifuatilia burudani
DJ Ray akifanya yake wakati wa mahafali hayo
Mgeni rasmi,Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akichangia shilingi 300,000/= wakati wa harambee ya kuchangia kununua thamani kwa ajili ya bweni la wanafunzi wa kike litakaloanza kutumika mwaka 2017 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano Kom sekondari
Wa pili kutoka kulia ni meneja wa benki ya CRDB Shinyanga Said Pamui akizungumza wakati wa harambee hiyo ambapo alichangia shilingi 500,000/=
Meneja wa benki ya CRDB Shinyanga Said Pamui alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi kuwafungulia akaunti benki watoto wao katika benki ya CRDB
Mwenyekiti wa bodi ya shule Peter Kuguru akizungumza wakati wa harambee hiyo na kuchangia shilingi 50,000/-
Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Tunafuatilia kinachoendelea....
Wazazi wakiwa eneo la tukio
Wazazi wa kike wakichangia wakati wa harambee hiyo 
Wazazi wa kiume nao hawakuwa nyumba katika harambee hiyo
Walimu nao hawakuwa tayari kupitwa
Vijana wanatoa burudani kwa kucheza
Mgeni rasmi ,ambaye ni afisa elimu mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akitoa hotuba yake wakati wa mahafali hayo ambapo pamoja na mambo mengine aliipongeza shule kwa kuwa na uongozi madhubuti/imara kwani hakuna migogoro ya kiutendaji aliyopokea.Hali kadhalika aliipongeza shule hiyo kwa kuendelea kufaulisha wanafunzi katika mitihani mbalimbali sambamba na kuwa na mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi
Kahundi aliwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi huku akiwataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaozesha wanafunzi
Wahitimu wakijiandaa kupokea vyeti.Wanafunzi waliofanya vyema katika masomo yao walipata zawadi ya vyeti na pesa
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea
Zoezi la kugawa vyeti linaendelea
Wapiga picha wakichukua matukio
Tunafutilia kinachoendelea hapa...
Wahitimu wakiendelea kupokea vyeti
Wazazi na walezi wakiwa kwenye mahafali ya 8 ya kidato cha nne Kom Sekondari mwaka 2016.



Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post