MIKOA INAYOONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA


Mikoa ya Tabora, Katavi na Rukwa imetajwa kuwa ni miongoni mwa mikoa 10 inayoongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi.


Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011/2012 za Taasisi ya Mkapa.


Taarifa hiyo ilitolewa na Meneja Mradi wa TB na Ukimwi kutoka Taasisi ya Mkapa, Dkt. Happenes Wilbroad katika mafunzo ya siku moja ya viongozi wa dini yaliyofanyika Nzega.


Alisema mkoa unaoongoza kwa maambukizi ya VVU kati ya mikoa hiyo mitatu ni Rukwa wenyeasilimia 6.2 ukifuatiwa na Katavi asilimia 5.2 na Tabora asilimia 5.1.


Dk. Wilbroad alisema Taasisi ya Mkapa imeanza kuendesha mafunzo ya kuhakikisha wananchi wanatambua na kuepuka maambukizi mapya.


Alisema jitiahada mbalimbali za kudhibiti maambukizi hayo zinapaswa kufanyika kunusuru maisha ya wakazi wa maeneo hayo.


Alitaja sababu zinazochangia maambukizi kuwa ni pamoja na ndoa za utotoni, tohara za jadi na baadhi ya wananchi kutozingatia elimu ya Ukimwi na kukithiri imani potofu za ushirikina.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post