Breaking News!! NOAH YAUA WATU 18 SHINYANGA BAADA YA KUGONGANA NA LORI..ANGALIA PICHA INATISHA SANA


Ajali ya Noah Nsalala Tinde Shinyanga Malunde1 blog
Noah ikiwa imeharibika-Picha zote na Frank Mshana- Malunde1 blog


Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Jumanne Muliro akiwa katika eneo la tukio

 Noah ikiwa imeharibika

Ajali ya Noah Nsalala Tinde Shinyanga Malunde1 blog
Miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio
Ajali ya Noah Nsalala Tinde Shinyanga Malunde1 blog
Noah ikiwa eneo la tukio



Ajali ya Noah Nsalala Tinde Shinyanga Malunde1 blog
Lori likiwa limeharibika
Ajali ya Noah Nsalala Tinde Shinyanga Malunde1 blog
Lori likiwa limeharibika
Ajali ya Noah Nsalala Tinde Shinyanga Malunde1 blog

Miili ya watu waliofariki dunia katika ajali ya Noah kugongana na lori


Ajali ya Noah Nsalala Tinde Shinyanga Malunde1 blog
Picha zote na Frank Mshana- Malunde1 blog 
*****
Watu 18 wamefariki dunia na watatu kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya Noah iliyokuwa inatoka Nzega mkoani Tabora kuelekea Tinde mkoani Shinyanga na lori aina ya Scania lililokuwa linatoka Kahama kuelekea Dar es salaam.


Ajali hiyo imetokea leo
Jumapili,November 06,2016 majira ya mbili kasorobo usiku katika eneo la Nsalala kata ya Tinde mkoani Shinyanga (Barabara ya Nzega- Shinyanga).

"Noah ilikuwa inataka kulipita lori jingine ndipo ikagongana uso kwa uso na lori lililokuwa linatoka Kahama... watu waliopoteza maisha papo hapo ni 15,watatu wamefariki wakati wakipatiwa matibabu,ajali inatisha,dereva wa Noah kajisalimisha kituo cha polisi Tinde",kimesema chanzo cha habari cha Malunde1 blog.

Majeruhi wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Hii hapa taarifa ya Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga




  “AJALI YA GARI KUGONGANA NA KUSABABISHA VIFO SHY/TR/AR/185/16.
 06/11/2017 MAJIRA KATI YA 1900 - 1930HRS KATIKA BARABARA YA NZEGA - TINDE, KATIKA KIJIJI CHA NSALALA KATA YA TINDE WILAYA NA MKOA WA SHINYANGA GARI NA T 232 BQR TOYOTA NOAH MALI YA MWINYI KHAMIS WA TINDE IKIENDESHWA NA SEIF S/O MOHAMED, 32YRS, SUKUMA NA MKAZI WA TINDE, IKITOKEA NZEGA KWENDA TINDE ILIGONGANA USO KWA USO NA SEMI TELLER T198 CBQ/T283 CBG  ILIYOKUWA IKITOKEA TINDE UELEKEO WA NZEGA MALI YA ALOYCE S/O KAVISHE, MCHAGA, 46YRS MKAZI WA DSM NA AMBAYE PIA ALIKUWA DEREVA WA GARI HILO NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 18.

 KATI YAO WANAUME 7 , WANAWAKE 9 NA WATOTO 02 WAKIKE WENYE UMRI WA KATI YA MIAKA 3- 5, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITAL YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA.

TUKIO HILI LIMEKAGULIWA NA ACP J. MULIRO KAMANDA MKOA WA SHINYANGA, SSP MWAKISAMBWE - RCO SHINYANGA NA SP ANTONY MASANZU - RTO SHY AKISAIDIWA NA DTO SHY ASP ANTONY GWANDU. 

MADEREVA WOTE MBARONI KWA MAHOJIANO  YA TUKIO HILO NA HATUA ZA ZAIDI ZA KISHERIA.

 CHANZO CHA AJALI HII KWA TAARIFA ZA AWALI NI UZEMBE WA DEREVA WA NOAH KUAMUA KUYAPITA MAGARI YALIYOKO MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI NA HATIMAE KUGONGANA USO KWA USO NA LORI - SEMITELLAR. MAREHEMU WATATU WAMETAMBULIWA”-RPC SHINYANGA MULIRO J.MULIRO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post