MSICHANA AJIUA BAADA YA KUMFUMANIA MPENZI WAKE AKIWA NA MPENZI MWINGINE HUKO RUVUMA



MKAZI wa mtaa wa Furaha Stoo Mbinga mjini mkoani Ruvuma Digna Chikuli (22) amefariki dunia baada ya kukutwa amejinyonga na mwili wake ukiwa unaning'inia chumbani kwake, katika dari ya nyumba aliyokuwa akiishi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma, Zubery Mwombeji alisema tukio hilo lilitokea Septemba 30 mwaka huu saa 4:00 asubuhi.

Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, baada ya Digna kumfumania mpenzi wake akiwa na mpenzi mwingine.

Alisema taarifa za kumfumania mpenzi wake huyo, zilitolewa na majirani wenzake wanaoishi katika mtaa huo na kwamba Digna alipotoweka katika eneo la fumanizi, ndipo baadaye walipata taarifa kuwa amejinyonga.

"Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya Mbinga, ukisubiri ndugu wauchukue kwa ajili ya taratibu nyingine za mazishi ili ziweze kuendelea kufanyika", alisema.

Imeandikwa na Muhidin Amri- Habarileo Mbinga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post