ALIYEVUMBUA NEPI " PADDI" AFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 94


Valerie Hunter Gordon na binti yake Frances katika tangazo la awali la Paddi


Valerie Hunter Gordon, katika picha mwaka jana, amefariki dunia kwake Beauly


Valerie Hunter Gordon, mama wa watoto sita aliyevumbua nepi za kutumiwa na kutupwa ameaga dunia nyumbani kwake karibu na Inverness akiwa na umri wa miaka 94.

Familia yake inasema alifariki October 16 huko Beauly.

Alivumbua nepi ya kwanza ya kutupwa iitwayo "Paddi" baada ya kumzaa mwanawe wa tatu Nigel, mnamo 1947 na baada ya kuchoshwa na kufua nepi za vitambaa.

nepi hizo awali zilitengenezwa kwa nyloni, karatasi na pamba.

Bi Hunter Gordon alitengeneza mamia ya nepi kwa kuzishona kwa cherehani jikoni kwake, na kuzisambaza kwa rafiki zake huku akizifanyia ukarabati mara kwa mara.

Mumewe, Meja Pat Hunter Gordon, alilazimika kumsaidia kutengeneza nepi hizo aliporudi kutoka vitani Borneo.
Nepi 'mbovu'

Akizungumza na BBC mnamo 2015, Bi Hunter Gordon amesema laiona kazi kubwa kufua nepi na ndipo akaanza kutafuta atakazoweza kutumia na baadaye kuzitupa.

"Nilidhani zauzwa - lakini zilikuwa hazipatikani kokote," alisema.

"Ilishangaza sana kwamba haizjawahi kutengenezwa. Nilidhani itakuwa rahisi kwahivyo wacha nizitengeneze. Lakini haikuwa rahisi, ilikuwa vigumu kiasi .

"Kila aliyeziona alisema, Valerie, tafadhali nitengeneze na mimi moja? Kwahivyo niliishia kutengeneza kama nepi 600.

"Niliishia kwenye cherehani cha mamangu, kutengeneza nepi hizi mbovu."

Paddis zilitumika badala ya nepi za tauli ,ambazo ilikuwa ni lazima uzioshe baada ya matumizi.

"Kila mtu alitaka kuacha kusha nepi. Sikuhizi ni kama wanataka kurudi kuzifua tena - kila la kheri kwao," alisema Bi Hunter Gordon mwaka jana.Tangazo kuhusu nepi za Paddi zilizovumbuliwa na Bi Hunter Gordon

Bi Hunter Gordon na mumewe walitia saini makubaliano na kampuni ya Robinsons mnamo 1948 kutengeneza nepi hizo 1949.

Miongoni mwa majina yaliofikiriwa kupewanepi hizo ni pamoja na Valette, Snappy, Napkins, Lavnets na Drypad. Jina Paddi lilichaguliwa baada ya mkutano kati ya Major Hunter Gordon na kundi la maafisa wakuu watendaji katika chuo cha uanajeshi Surrey, kwa mujibu wa mtandao wa Paddi.

Awali madaktari walikuwana shaka nazo nepi hizo, waliodhani zitawadhuru watoto.

Hata hivyo ripoti katika jarida la Lancet iliyoandikwa na daktari wa jeshi aliyemtumilia mwanawe Neppi hizo, ilisaidia kubadili mtazamo wa kitabibu na zikaanza kuuzwa katika maduka ya BootsZilitangazwa kama nepi zilizo nzuri na zilizoundwa na mama kwa ujuzi.

Kampuni hiyo ilifungwa katika miaka ya 1960, kufuatia kuzuka kwa Pampers kutoka Marekani.

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post