Mganga wa Jadi Mbaroni Kwa Tuhuma ya Kumbaka Binti Mteja Wake Huko Kigoma ,Alimwambia Akifanya Naye Tendo la Ndoa Lazima Apone Masikio
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia Hamza Saidi,(40) mganga wa jadi mkazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji kwa tuhuma za kumbaka binti mwenye umri wa miaka (20) aliyefika nyumbani kwake kupata tiba ya masikio.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma SACP Fredinand Mtui alisema, mnamo Mei 15, 2015 majira ya saa 11:20 huko ujiji katika Manispaa hiyo binti mmoja (Jina linahifadhiwa) Mkazi wa Ujiji alifika nyumbani kwa mganga huyo akiwa anaumwa masikio kwa lengo la kupata tiba.Mtui alisema baada ya binti huyo kufika kwa mganga na kumueleza tatizo lake mganga huyo alimwambia kuwa ili dawa iweze kufanya kazi lazima afanye naye tendo la ndoa ili dawa hiyo iweze kufanya kaz.
Alisema mtuhumiwa wa tukio hilo ameshikiliwa na atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria zaidi.


Katika tukio lingine mnamo Mei 14, 2015 katika kata ya Kagera Nkanda Tarafa ya makere Josephine Ntahukisiga (42) mkulima mkazi wa Mvinza alikutwa akiwa amejinyonga ndani ya nyumba ya baba yake kwa kutumia shuka.


Ntahukisiga alivizia ndugu zake wakiwa wamelala ndipo alipoenda sebuleni na kujinyonga kwa kutumia shuka kwa kulifunga juu ya dali.
 Kwa mujibu wa baba yake Andrew Ntahukisiga alisema marehemu alikuwa na msongo wa mawazo tangu watoto wake walipofariki kwa ajali ya moto mwaka 2015.

Na Rhoda Ezekiel-Malunde1 blog Kigoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post