SERIKALI NA WADAU WATAKIWA KUPAMBANA NA UDUMAVU WA WATOTO TANZANIA


Juhudi za pamoja ikiwemo serikali na wadau mbali mbali zinahitajika katika kupambana na udumavu wa watoto Tanzania unaotokana na utapiamlo mkali ili kujenga Taifa lenye watoto wenye afya njema na uwezo mkubwa wa kiakili.



Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania( PANITA) yanashughulikia utetezi na ushawishi wa lishe bora nchini Bw. Tumaini Mikindo katika mafunzo za ya uboreshaji wa shughuli za PANITA kwa waratibu wa kanda kumi nchini Tanzania yaliyofanyika mjini Morogoro juzi.



Bw. Mikindo amesema takwimu zilizotolewa na TDHS kwa mwaka 2010 zinaonyesha kuwa 42% ya watoto wa Tanzania wameathirika kwa udumavu kutokana na utapiamlo mkali jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza uwezo wa kufikiri na hatimaye watoto kushindwa kufanya vizuri shuleni.



Mkurugenzi huyo wa PANITA ameongeza kuwa kimsingi mtoto anaposhindwa kufikiri vizuri na hatimaye kufanya vibaya katika masomo mtiririko wake unalete madhara hata katika suala zima la kiuchumi na hivyo inakuwa ni vigumu kupambana na umaskini kwani uwezo wake wa kuchambua mambo kwa usahihi unakuwa mdogo.



Mikindio ameongeza kuwa upo umhimu mkubwa wa kuzingatia siku 1000 za toka mimba inavyotungwa hadi mtoto kufikia umri wa miaka 2 katika kuzingatia suala zima la lishe bora kwani ni kipindi muhimu katika makuzi ya mtoto na huo ndio wakati ambao msingi wa ukuaji wa mtoto kiakiri na kimwili unapojengwa.



Akizungumzia madhara ya utapiamlo kwa watu wenye umri mkubwa mkurugenzi huyo amefafanua kuwa watu wenye umri mkubwa waliozaliwa na uzito pungufu(chini ya kilo mbili nusu) kutokana na lishe duni wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kisukari.



Kufuatia hali hiyo Bw. Mikindo amewataka wanachama wa PANITA nchini na wadau mbali mbali hali kadharika serikali kuisadia jamii katika kuelimisha umuhimu wa lishe bora na hatimaye kuondokana na tatizo la utapiamlo.



Warsha hiyo ya siku 3 iliyoandaliwa na PANITA iliwashirikisha waratibu wa PANITA kutoka katika kanda 10 nchini Tanzania ambapo ililenga kuwakumbusha waratibu hao majukumu yao ,mbinu mpya za kutambua tatizo na ufumbuzi wake.

Na Frank Kasamwa-Morogoro

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527