KUHUSU KESI YA LEMBELI KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU 2015 HUKO KAHAMA





Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka jana iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Kahama mjini Bw.James Lembeli dhidi ya mgombea wa CCM Mh.Jumanne Kishimba imeendelea leo katika mahakama ya wilaya ya Kahama.
 
 
Kesi hiyo amnbayo iliendelea kuunguruma leo majira ya saa tano kamili huku wananchi waliofika mahakamani hapo kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo wakiilalamikia mahakama kutoweka vipaza sauti hali inayosababisha idadi kubwa ya wananchi waliofika kusikiliza kesi hiyo kushindwa kuelewa nini kinaendelea.
 

Aidha baada ya jaji Moses Mzuna kusikiliza hoja za kila upande na kuridhika na maelezo aliagiza pande zote mbili kuleta mashahidi wao ili waanze kutoa ushahidi na kuahirisha kesi hadi kesho siku ya Jumatano tar.02/03 ambapo kesi itaendelea.
 Via>>>ITB

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post