HIZI NDIYO NCHI 10 DUNIANI AMBAZO HAZINA FURAHA,TANZANIA NAYO IMO

Denmark imechukua nafasi ya Switzerland kama nchi yenye furaha zaidi duniani kwa mujibu wa ripoti iliyotoka wiki hii.

Ripoti hiyo imeandaliwa na ‘Sustainable Development Solutions Network and the Earth Institute’ katika chuo kikuu cha Columbia.

Ilionesha kuwa Syria, Afghanistan na nchi zingine 8 zilizopo chini ya jangwa la Sahara ndizo sehemu zisizo na furaha zaidi. Nchi hizo ni pamoja na Madagascar, Tanzania, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Togo na Burundi.

Nchi 10 za juu zenye furaha zaidi ni Denmark, Switzerland, Iceland, Norway, Finland, Canada, Uholanzi, New Zealand, Australia na Sweden.

Nchi tano duniani, Bhutan, Ecuador, Scotland, UAE na Venezuela zimeteua mawaziri watakaoshughulikia ukuzaji wa furaha.

Tanzania tuna matatizo gani? Kuna umuhimu wa Magufuli kuanzisha wizara kama hiyo pia?

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527