LOWASSA : MAGUFULI NI MIONGONI MWA MARAIS WA AFRIKA WASIO NA MAONO"

Edward Lowassa leo ameamua kumuelezea ukweli rais Magufuli kuwa ni miongoni mwa marais wa Afrika wasio na maono. Lowassa pia amesema kuwa Tanzania chini ya Magufuli itakosa kabisa ubunifu.


Hayo yanajiri baada ya rais John Magufuli kuzuia mambo mengi kwa lengo la kubana matumizi. Huku wataalam mbalimbali wakikwama kuwekeza kwenye taaluma baada ya kuzuiwa kupata mafunzo mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Aidha rais Magufuli amekuwa akitoa hotuba kwa hisia kali hali inayowafanya wasaidizi wake kuingiwa na woga kwenye uthubutu.

"Magufuli amewafanya wasaidizi wake kukosa kabisa ubunifu na uthubutu wa kufanya maamuzi. Tanzania chini yake haitakuwa na jipya" amesema Lowassa.

Aidha Lowassa amesema kuwa sera ya elimu bure kwa Magufuli imekuwa "zero" baada ya kuiga. 
Chanzo-Udakuspecially.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post