HII NDIYO SABABU YA MBUNGE KUFUKUZWA BUNGENI DODOMA
Mwenyekiti wa Bunge Mh Andrew Chenge ameamuru kutolewa nje kwa Mh Jesca Kishoa mbunge wa viti maalum Singida na kutohudhuria vikao vyote vilivyobaki katika mkutano huu wa pili kutokana na kushindwa kuthibitisha kauli aliyoitoa bungeni kuwa aliyekuwa waziri wa uchukuzi Mh Dk Harrison Mwakyembe ameisababishia serikli hasara ya shilingini bilioni 238 fedha ambazo zilitumika kununulia mabehewa feki.

Mwenyekiti Chenge ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya kusoma taarifa ya spika ambapo Mh Jesca alitakiwa kuifuta kauli yake aliyoitoa bungeni wakati akichangia february mosi katika hotuba ya waziri wa fedha kuhusu mpango wa maendeleo wa serikali lakini Mh Jesca akakata kufanya hivyo. 

Baada ya kutolewa nje ITV ilimtafua Mh Jesca kwa lengoa la kujuwa alikwama wapi kuwasilisha ushaidi wake na kusema kuwa aliziandikia ofisi huska ikiwemo ofisi ya bunge kuomba ripoti ya PPRA ambayo ndio yenye ushaidi huo lakini hawakumpa ushirikiano.

Kama kawaida wabunge waliendelea na mjadala wa mpango wa maendeleo wa serikali ambapo Mh Doto Biteko mbunge wa Bukombe amesema mpango huo lazima utoe fursa kwa vijana kupata maeneo ya kujiajiri ambapo Mh Godfrey Mgimwa mbunge wa Kalenga amesema serikal iongeze vyanzo vya mapato kupitia sekta ya uvuvi.

Katika hatua nyingine Mh Zitto Kabwe alitaka serikali itoe tamko kuhusu sakata la mwanafunzi wa kitanzania kudhalilishwa kwa kutembezwa uchi nchini India baada ya kutokea vurugu katika mitaa ya Bangalore ambapo serikali imesema imeanza kulifanyia kazi jambo hilo ikiwemo kuuandikia ubalozi wa India kwa lengo la kuonyesha kusikitishwa na tukio hilo.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post