RAIS MAGUFULI AMEMWAGA MABILIONI YA FEDHA KWA AJILI YA WANAFUNZI WA TANZANIA,SASA NI RASMI ELIMU BURE




KIASI cha shilingi bilioni 18.77 zimetumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini kwa ajili ya wanafunzi kusoma bure.


Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.


Pesa hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na bilioni 3 kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri zote hapa nchini.


Dk.Mipango amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika kwa matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.


Pia Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Mipango amewaomba waalimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini waweke wazi matumizi ya fedha hizo katika mbao za matangazo kwa kila shule ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Beno Nduru akifafanua jambo kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Kulia Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha na Mipango, Servacius Likwelile.

Kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusiana na ukusanyaji wa mapato katika Malaka ya Mapato Tanzania kwa kila robo mwaka.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango jijini Dar es Salaam jana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527