Majanga Katavi!! KAKA AUA KWA FIMBO KIJANA ALIYEMFUMANIA AKITONGOZA DADA YAKEMkazi wa Kijiji cha Kalovya Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mele Ramadhani Ally (26) amefariki dunia wakati akiwa anapatiwa matibabu kufuatia kipigo kikali alichokipata kutoka kwa Ntemwa Kabembanya(26) Mkazi wa Kijiji cha Ipwaga Tarafa ya Inyonga baada ya kukutwa barabarani akiwa anaongea/kutongoza dada wa mtuhumiwa wa tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa kumi na mbili na nusu katika Kijiji cha Ipwaga.

Siku hiyo ya tukio mtuhumiwa Ntemwa alimkuta marehemu akiwa amesimana dada yake aitwaye Ngoro Mbogo (12) huku wakiwa wanaongea .

Kamanda Kidavashari aliwaambia Waandishi wa Habari kitendo hicho cha kuwakuta wakiwa wamesimama huku wakiwa wanaongea kilimkasirisha sana mtuhumiwa .

Ndipo pasipo kumwambia neno lolote alianza kumshambulia kwa kumpiga na fimbo katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku dada wa mtuhumiwa akiwa anashuhudia kipigo hicho.

Alisema mtuhumiwa aliendelea kumshambulia na marehemu alipoona kipigo kimzidia alianza kupiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo na kumkuta marehemu akiwa hoi .

Na walimchukua na kumpeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Mlele kwa ajiri ya kupatiwa matibabu na alipofikishwa hapo alilazwa wodini kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Kamanda Kidavashari alisema wakati akiwa anaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali hiyo alifariki dunia .

Alieleza kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa Ntemwa Kabembanya na anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika ili akajibu tuhuma inayo mkabil.

Na Walter Mguluchuma-Malunde 1 blog Katavi

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527