HAPA KAZI TU!! RAIS MAGUFULI AMPIGIA SALUTI MBWANA SAMATTA,ATUMA SALAMU ZA PONGEZI


 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salam za pongezi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Mbwana Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Barani Afrika; iliyotolewa katika mji wa Abuja nchini Nigeria jana usiku..


Mhe. Rais Magufuli amemtaka Waziri Nape Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Amesema tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.


Aidha, Rais Magufuli amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo kuongeza juhudi za kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za kimaendeleo.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
08 Januari, 2016

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527