BAADA YA WAZIRI NAPE NAUYE KUTUMBUA JIPU LA STAND UNITED..HAYA NDIYO YAMEJIRI LEO SHINYANGA..CLOUDS FM NA RADIO FREE AFRICA VYALAUMIWA KUIVISHA JIPU





Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo leo kumefanyika kikao cha wadau wa michezo mkoani Shinyanga kwa ajili ya kukabidhi timu hiyo kwa viongozi wa Stand United kupitia kamati ya muda na kuzungumzia mstakabali wa kuisadia timu ya Stand United ili ipate mafanikio zaidi.Kikao hicho kilikuwa kinaongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga(pichani katikati).Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau wa michezo,Kamati ya maridhiano ya uendeshaji wa timu ya Stand United iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga yenye wajumbe sita,Viongozi wa soka mkoa wa Shinyanga na TFF.


Hata hivyo katika hali iliyozua sintofahamu viongozi wa Stand United wala wajumbe wa Kamati tendaji ya muda ya Stand United wakiongozwa na mwenyekiti wao Amani Vicent ambao siku chache zilizopita walikwenda kwa waziri wa michezo Nape Nnauye kulalamika kuhusu kamati iliyoundwa na mkuu wa mkoa kuwa wanafanya ubadhirifu wa fedha za wadhamini ACACIA,Nape akatoa tamko kuwa wanachama wa Stand United warudishiwe timu yao,hawakuhudhuria kikao hicho huku kukiwa na taarifa kuwa walikuwa wanachungulia kwenye ukumbi huo bila kuingia ndani-Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea habari picha...angalia hapa chini



Wadau wa michezo mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini,ambapo pamoja na mambo mengine viongozi wa Kamati ya maridhiano ya uendeshaji wa timu ya Stand United iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga walitumia fursa ya kikao hicho kueleza kuwa mgogoro ndani ya timu hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari na kuitaja Clouds fm na Radio Free Africa waziwazi kuwa wamekuwa vikitumika kuchochea mgogoro ndani ya timu ili kuvunja maendeleo ya udhamini uliopatikana.



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizungumza katika kikao hicho cha wadau wa michezo,ambapo alisema vyombo vya habari ikiwemo Clouds fm vimekuwa vikitumika kuleta mgogoro katika timu hiyo.Hata hivyo Rufunga alisema hajaanza leo kusemwa/kuandikwa,wala haogopi kusemwa na vyombo vya habari wataoendelea kumsema ni sawa na kumpaka marashi hivyo wanafagilia tu kwa ajili ya uteuzi ujao



Rufunga alisema changamoto kubwa mkoani Shinyanga ni majungu huku akiwataka viongozi wa Stand United kuzingatia masharti ya wadhamini wao ACACIA kuwa timu ikishuka nafasi ya sita hawaidhamini tena.Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema kama hesabu ya vurugu ya baadhi ya viongozi wa Stand United waliokwenda kwa waziri Nape Nnauye ni tamaa ya fedha basi wamekosea fomula,bali wangebuni njia nyingine kwani serikali mkoani Shinyanga haiko tayari kuona fedha za wadhamini zinatumika ndivyo sivyo.Hata hivyo amemuagiza katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga kusimamia zoezi la kukabidhi nyaraka muhimu kwa viongozi wa Stand United kabla ya siku ya Jumamosi wiki hii



Wadau wakiwa ukumbini



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza katika kikao hicho,ambapo alisema mkoa wa Shinyanga una mpango wa kuwa na timu kubwa kila wilaya na tayari sasa kuna timu mbili ambazo ni Stand United na Mwadui FC huku akiwataka wadai wa michezo kuungana pamoja ili kufanikisha maendeleo ya timu za mpira mkoani humo


 

Mkuu wa mkoa Ally Rufunga alisema lengo la kuunda kamati ya mkoa ilikuwa ni kusimamia timu hiyo ili iweze kufadhiliwa na iweze kusonga mbele,kwa vile wameamua kutoihusisha serikali aliwataka viongozi waliokwenda kwa waziri michezo Nape Nnauye waje kukabidhiwa timu yao kabla ya siku ya Jumamosi na wasipofika atawatafuta mwenyewe.



Mratibu wa kamati ya timu ya Stand United Mbasha Matutu,iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga, akizungumza kwenye kikao maalumu cha kujadili mustakabali wa maendeleo ya timu hiyo, ambapo alisema timu hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kocha kuingiliwa majukumu yake na changamoto hizo zimekuwa zikisababishwa na kikundi kidogo chenye nia mbaya na maendeleo ya timu hiyo, ambacho kinajiita kuwa kina uchungu na timu hiyo
ambacho hakipo hata kwenye orodha ya waanzilishi wa timu hiyo.



Matutu alisema watu wenye kikundi hicho ambao wanajiita wenye timu ni
Bakari Mfundo, Said Mponda Mponzemanya Mevu, Moses Leji, Seif Hamad,Daud Lef, Ibrahim Mfundo na Omari Maburuki ambao wamekuwa wakisababisha matatizo mbalimbali kwenye timu hiyo na kuisababisha kushindwa kusonga mbele.

Matutu alisema kikundi hicho kimekuwa kikiwachanganya wachezaji ili washindwe kucheza vizuri wafungwe ambacho kiongozi wake ni Seif Hamad ambaye ni mtumishi wa serikali na Bakari Mfundo ambapo wamekuwa wakimsababisha kocha wa timu hiyo kukosa amani kwa kujengewa hofu
katika kazi zake.



Pia Matutu alisema kikundi hicho cha watu wachache kimekuwa kikipora mapato ya mlangoni na kukiuka utaratibu wake uliowekwa na kamati ya uendeshaji wa timu kwamba fedha zote za “get collection”zikusanywe na zipelekwe benki.



Matutu pia alivinyoshea kidole vyombo vya habari kwa kujiingiza katika mgogoro wa timu hiyo huku akisisitiza kuwa Clouds Fm na Radio Free Africa vimehusika kwa kiasi kikubwa kuchochea mgogoro huo wakitumiwa na kundi la baadhi ya watu katika timu hiyo



Waandishi wa habari wakiwa ukumbini



Msemaji wa Stand United Deo Kaji Makomba akizungumza katika kikao hicho,ambapo alisema kitengo cha habari kimekuwa kikiingiliwa katika utendaji wa kazi nje




Makomba alisema vyombo vya habari vimekuwa vikitumiwa vibaya kuchochea mgogoro ndani ya timu hiyo..TAARIFA YAKE IKO HAPO CHINI YA PICHA ZOTE



Kocha mkuu wa Stand United Patrick Liewig akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema yeye anataka timu isonge mbele hataki mambo mengine yale yaliyojitokeza ameyasamehe
yote na anachohitaji ni  kuhakikisha timu inasonga mbele



Boniface Wambura kutoka TFF akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema Stand United lazima isonge mbele na kila mtu atoe ushirikiano kwa timu hiyo huku akiwataka viongozi na wachezaji wa timu hiyo kuzingatia masharti ya wadhamini wao


Mwenyekiti wa chama cha Soka mkoa wa Shinyanga Benister Lugola akizungumza katika kikao hicho

IFUATAYO NI TAARIFA YA IDARA YA HABARI KATIKA TIMU YA STAND UNITED ILIYOTOLEWA NA MSEMAJI WA TIMU HIYO DEO KAJI MAKOMBA





Hata hivyo akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu,mwenyekiti wa Stand United Amani Vicent amesema hawajahudhuria kikao cha wadau kilichoitishwa na mkuu wa mkoa hawakuhudhuria kikao hicho kutokana na uongozi wa mkoa kutofuata taratibu za makabidhiano ya nyaraka

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527