WABUNGE WA UKAWA WASEMA WATAFANYA MAAMUZI MAGUMU KAMA RAIS MAGUFULI ATAINGIA NA DR SHEIN BUNGENI IJUMAA




Wabunge wanaotoka katika vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi -UKAWA wamesema watafanya maamuzi magumu siku ya Ijumaa iwapo Rais Dr.John Magufuli ataambatana na Rais wa Zanzibar Dr.Ally Mohamed Shein katika ufunguzi wa bunge huku viapo vya wabunge wateule wengine vikiendelea.



Wakizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge, Viongozi wa wabunge hao wamesema kuruhusiwa kwa Dr.Shein kuingia ndani ya bunge siku hiyo ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar na tayari wamemwandikia barua spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai kumtahadharisha juu ya ujio wa Dr.Shein.

Baadhi ya wabunge watokao ndani ya umoja huo wamesema matatizo yanayoikumba Zanzibar kwa sasa yatokanayo na kauli ya Tume ya Taifa ya Zanzibar kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar ni ya Tanzania yote kwa kuwa Zanzibar ni sehemu ya Muungano.

Katika hatua nyingine wabunge wateule wameendelea kuapa ili waweze kuwa wabunge kamili.

Baadhi ya wabunge wapya na wale wa Zamani ambao wameapa wamesema watahakikisha wanalitumika Taifa la Tanzania kikamilifu na kuwaondolea kero sugu zinazowakabili.

Via>>itv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post