Ni stori iliyoanza kuchukua nafasi kubwa sana katika mitandao mbalimbali usiku wa kuamkia October 16 2015 headlines za siasa Tanzania zimetawaliwa na ajali ya Helikopta ambayo imeanguka na kulipuka kwenye mbuga ya Wanyama ya Selous ambapo Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alithibitisha kwamba mmoja wa waliokuwemo ndani ni Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM).
Sasa leo baada ya masaa kadhaa mgombea Ubunge kupitia chama cha CCM jimbo la Ukonga Jerry Silaa alipost picha ya Helicopter na kuandika maneno kuhusiana na ajali hiyo.
>>>Baba yangu Capt.William Silaa akiwa na Mhe.Deo Filikunjombe na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya helicopter 5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa. Taarifa za mwisho ilionekana imeanguka kwenye msitu wa Selous.
Hakuna mawasiliano ya simu. Usiku kucha vyombo vyote vya serikali vimeendelea na jitihada za kufika eneo la tukio na jitihada kubwa zaidi zinaendelea asubuhi hii – Jerry Silaa
‘Nawaomba wote kuwa watulivu kwani jambo hili linahitaji umakini wa hali ya juu na ushirikiano wa taasisi nyingi za wizara tofauti.Tuwaombee wote Mungu awanusuru‘ – Jerry Silaa
Baada ya hapo tukapata maelezo kutoka kwa Waziri wa Utalii na Maliasili, Lazaro Nyalandu akasema…>>Tumeipata hiyo taarifa lakini hatufahamu kinachoendelea tunaamini kwamba Mungu atafanya miujiza juhudi za kuwapata nafikiri muda si mrefu tunaweza tukafanikiwa, changamoto iliyosababisha watu wa msaada kuchelewa kufika kwenye eneo la Ajali moja taarifa za hiyo ajali tulizipata wakati giza lilikuwa limeshaingia hilo la kwanza, la pili ajali hiyo imetokea katika kitalu cha wawindaji kinachojulikana kama R3 na walioshuhudia walikuwa katika kitalu R2 tofauti yao ni kwamba wametenganishwa na mto ambao unaenda kwa kasi halafu una mamba. Sisi tulichokifanya kama Serikali ni kwamba tumetuma kikosi kimoja ambacho kilikuwa kina askari nane na RPC wa Morogoro pia naye akawatuma maskari kwenda kwenye eneo hilo la ajali kwa hiyo lazima tufahamu kwanza helikopta ilipodondoka na tutambue kama kutakuwa na wale ambao watakuwa wamenusurika au wako wapi na leo Asubuhi tumetuma helikopta kuangalia kile kinachoendelea kwa hiyo tunasubiri taarifa za huko watakaporudi kwani sehemu ambayo walipo hakuna hata mawasiliano ya simu.
Taarifa tulizozipata kutoka kwa mashuhuda wa eneo hilo kwa wawindaji mahiri walipiga simu kwa njia ya Satelite na kusema kwamba wameona helikopta moja imeanguka msitu wa Selous kwenye kitalu R3 mto Ruaha baada ya hapo wakaona moto kwa hiyo sisi kama Serikali tunaendelea kufanya uchuguzi wa kina- Lazaro Nyalandu.
SOMA HABARI KAMILI HAPA
Social Plugin