UPDATES ZAIDI ZA KIFO CHA WAZIRI CELINA KOMBANI

Usiku wa September 24 2015 taarifa ya Majonzi imesambaa na kuwafikia watu kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari pamoja na mitandao ya Kijamii, Serikali ikathibitisha pia kuhusu msiba wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mama Celina Kombani amefariki Dunia kutokana na maradhi ya Saratani, na amefariki akiwa India ambako alienda kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
E83A4560
Kuhusu taratibu zinazofatia, nimeipata taarifa kutoka Ofisi za Bunge ambapo inaonesha mipango ya kusafirisha mwili wa Marehemu mpaka Dar es Salaam inafanyika na mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Dar Jumatatu September 28 2015, na baadae msiba utasafirishwa kupelekwa Mahenge Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya mazishi.
Marehemu Mama Celina Kombani amefariki akiwa na umri wa miaka 56 na alikuwaWaziri na pia Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki.
 
Nimepokea kwa majonzi makubwa taarifa ya msiba wa Mama Celina Kombani. Nawapa pole wananchi wa Ulanga Mashariki na Chama…

RIP Mama Celina Kombani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527