Ajali! TRENI MBILI ZAGONGANA KISHA KUTUMBUKIA MTONI NA KUUA WATU 24

ajalii

Ajali ambazo huripotiwa kila wakati nyingi ni zile zinazohusisha magari barabarani, lakini ajali za angani, majini na za treni hutokea lakini si kila wakati.
Huku India hakuishiwi matukio, kuna hii ajali nyingine imetokea usiku wa kuamkia leo baada ya treni mbili kukosea njia na mabehewa sita kutumbukia mtoni na kusababisha vifo vya watu 24.
Treni hizo zilitumbukiwa katika mto uliokuwa umejaa maji kutokana na mvua kubwa kuendelea kunyesha katika jimbo la Madhya Pradesh, na kusababisha idadi hiyo ya vifo na watu zaidi ya 300 kuokolewa.
Shirika la habari la India limesema ajali hiyo imetokana na treni hizo zilizopoteza mwelekeo kutokana na mafuriko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post