WATANO WAPOTEZA MAISHA BAADA YA MAGARI MAWILI KUGONGANA HUKO GEITA


Watu 5 wamefariki dunia papo hapo  na wengine watatu wamejeruhiwa wilayani Bukombe Mkoani Geita mara baada ya magari mawili kugonganana uso kwa uso katika kijiji cha Ishororo kata Bukombe mkoani humo.

Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 12 jioni ikihusisha magari mawili aina ya Toyota yenye namba T-302-DDT na T-402-CQJ, huku chanzo kikidaiwa kuwa mwendokasi uliosababisha madereva hao kushindwa kuchukua tahadhari.

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya wa Bukombe Mkoani Geita Dk. Daniel Sulusi amethibitisha kupokea maiti 5 na majeruhi watatu ambao amesema hali zao ni mbaya. 
Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia DUNIA KIGANJANI BLOG kuwa endapo madereva hao wangekuwa wanaendesha magari hayo mwendo wa kawaida wangeweza kuepusha ajali hiyo kwani eneo hilo linapitika vizuri na halina kikwazo chochote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post