News Alert !! FUSO LAGONGA HIACE MTONI,WATU WANNE WAFARIKI,MAJERUHI 11 HUKO KILIMANJARO

Gari aina ya Hiace iliyogongwa kwa nyumba na Fuso na kuuwa watu huko Moshi


Gari aina ya Hiace iliyogongwa kwa nyumba na Fuso na kuuwa watu huko Moshi


Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa watu wanne wamefariki dunia papo hapo na wengine 11 wamejeruhiwa baada ya gari dogo aina ya hiace waliyokuwa wakisafiria kugongwa na fuso katika eneo la mto Kikavu wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Fulgence Ngonyani amesema ajali hiyo imetokea mapema leo baada ya Fuso hilo ambalo lilikuwa nyuma ya hiace hiyo zote zikielekea mjini Moshi kuongeza kasi katika mteremko huo na kugonga gari hilo la abiria kwa nyuma.


Kamanda Ngonyani amesema Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Hai, na kwamba majeruhi wote wamepelekwa katika hospitali ya mkoa Mawenzi na wengine katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi.


Kamanda Ngonyani amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa Fuso hilo, na kwamba dereva wa Fuso hilo amekimbia mara baada ya kusababisha ajali hiyo.


Muonekano wa hiace baada ya ajaliEneo la tukioLori lililosababisha ajali
eneo la tukio

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post