MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA BANGO AKICHUNGULIA DIRISHANI KWENYE BASIWalioshuhudia mkasa huo wanasema mvulana huyo alikuwa anachungulia nje ya dirisha wakati basi alimokuwa lilipita katika barabara nyembamba nchini Afrika Kusini.

Polisi wameliziba eneo hilo na kuufunika mwili na mablanketi kabla ya kuondolewa kupelekewa katika chumba cha kuhifadhia maiti

Mvulana huyo ambaye bado hajajulikana wazi ni nani ni miongoni mwa kundi la wanafunzi 106 kutoka shule ya upili ya Molapo.

Maafisa wanachunguza kisa hicho kwa makini.

Wanafunzi wenzake na walimu wanaosemekana kufadhaishwa mno, wanapokea ushauri.

Mlinzi mmoja aliyekuwa katika eneo hilo ambaye ameomba asitajwe, alikuwa ameketi nje ya duka linalouza magari karibu na eneo hilo.

" Basi liligonga bango hili kwanza, kila mtu alikuwa ndani... Kisha mvulana alitoa kichwa nje ya dirisha alikuwa ameketi karibu na nyuma- alijaribu kuona kilichokuwa kinafanyika, na muda sio muda, aligongwa na bango hilo,"ameliambia gazeti la Durban Mercury.

"Kila mtu alikuwa analia, walimu, wanafunzi; kulikuwa na kizaazaa. Nilitaka kusaidia lakini sikuweza. Bado alikuwa anapumua - damu zilimvuja - nilipomfikia. Lakini sikuweza kumfanyia chochote," alisema shahidi mwingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post