MPAMBE WA LOWASA MZEE KINGUNGE ADAI CCM WALICHEZA RAFU MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA URAIS



Mwanasiasa mkongwe nchini na moja kati ya waasisi wa chama cha mapinduzi mzee Kingunge Ngombaru Mwiru amesema mchakato wote uliotumika katika kumpata mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM mwaka huu ulikuwa batili.


Akizungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, mwanasiasa huyo mkongwe hapa nchini kupitia chama tawala mzee Kingunge Ngombaru Mwiru, amesema mchakato wa kumpata mgombea wa urais ulikuwa batili kutokana na kamati ya maadili ambayo ni chombo cha kutoa ushauri kufanya kazi ya kamati kuu ambayo ni kutoa maamuzi, hivyo kamati ya maadili yenyewe ilishiriki kuvunja maadili.

Mwanasiasa huyo amesema kwa mujibu wa utaribu uliowekwa, wagombea wote wangetakiwa kupita mbele ya kamati kuu na kujieleza na kuulizwa maswali lakini haikufanyika hivyo, jambo ambalo si sawa huku akiongeza kuwa kuna watu walikuwa na orodha ya watu wao kuhusu nafasi ya urais.

Kuhusu ndugu Edwaed Lowasa, Kingunge amesema hausiki katika kashfa yeyote ya ufisadi kwa maana yeye aliwajibika kisiasa na si kwamba alihusika katika kashfa ya Richmond.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post