KOCHA MKUU WA TIMU YA TAIFA ATIMULIWA KAZI

kekee

Shirikisho la soka Nigeria NFF baada ya kupitiwa taarifa za Kamati ya Nidhamu, Ufundi na Maendeleo. limefikia uamuzi wa kumtimua kazi kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Super Eagles’, Steven Keshi kuendelea kuifundisha timu hiyo.

Makamu wa kwanza wa Rais wa NFF, Seyi Akinwunmi amewahakikishia Wanigeria kwamba uamuzi huo haujachukuliwa kwa kukurupuka, bali umezingatia maslahi ya soka ya Nigeria.

Keshi, ambaye ni Nahodha wa zamani Super Eagles amekuwa kocha wa timu ya taifa kwa vipindi vitatu tofauti kati ya mwaka 2011 na 2015, na mafanikio yake makubwa yakiwa ni kuwapa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 Afrika Kusini na kufika Raundi ya Pili katika Kombe la Dunia mwaka jana Brazil.

Kocha huyo amefukuzwai ikiwa ni miezi miwili kabla ya Nigeria kusafiri kuja Tanzania kumenyana na Taifa Stars katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwaka 2017.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post