BIASHARA YA NGONO YASHAMIRI MARADUFU MSIMU HUU WA URAIS CCM HUKO DODOMA



BIASHARA ya ngono imeshamiri mkoani Dodoma wakati huu ambao vikao vya kumpata mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimekwisha kuanza.

Uchunguzi uliofanywa katika baadhi ya kumbi kama Club Maisha, Club Laazizi na Matei Lounge, Chako ni Chako, umebaini kuwapo idadi kubwa ya kina dada wakiwa wamevaa nusu uchi.

Katika maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma zilikuwapo hekaheka za wasichana wanaojiuza ambao walionekana wakitafuta wateja bila ya wasiwasi wowote na wengine walisikika wakisema wako kibiashara na siyo kuuza sura.

Eneo maarufu la Chako ni Chako kuanzia jioni mpaka usiku kucha akina dada hao wamekuwa wakijazana hadi kwenye taa za kuongozea magari huku wakitafuta wateja wenye magari.

Baadhi yao ambao hawakutaka kutaja majina yao halisi mmoja wao alisema, ‘’Kaka sema una shilingi ngapi habari ya majina unataka kutupeleka wapi…?

‘’……wewe unaona shimo limetema hapa kila nikigeuka mwanaume na wanatoa ‘mpunga’ nadhani huyu rais ajaye atakuwa na neema.’’

Dada mwingine ambaye aliyekuwa Dodoma Carnival karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi, alisema ametoka Arusha akiwa na marafiki zake kwa lengo la kuwafuata wateja wa msimu walioko Dodoma.

Alisema hadi sasa ana siku tatu akiwa Dodoma na tayari amekusanya zaidi ya Sh 700,000 huku akiwatumia madalali ambao huwaunganisha kwa wateja ‘wazito’ (wenye fedha) kwa ujira maalum.



chanzo-Kibonaro

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post