Tukio la Ajabu!! MAMA AMLA MTOTO WAKE AKIWA HAI,ATAFUNA KIUNGO KIMOJA BAADA YA KINGINE

Kumekuwepo na matukio ya baadhi ya wazazi kuwanyanyasa na hata wengine kuripotiwa kuwaua watoto wao wa kuwazaa wenyewe kutokana na sababu mbalimbali.

Headlines nyingine leo zinatokea kule India ambapo mama mmoja amefunguliwa mashtaka baada ya kuripotiwa kumla mtoto wake wa miaka minne huku akiwa hai.

Pramila Mondal ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili alifanya kitendo hicho akiwa nyumbani kwake na kukutwa na shemeji yake akiendelea kumla mtoto huyo sehemu mbalimbali za mwili wa mtoto wake huyo ambaye alikuwa wa kike.

Baada ya Polisi kufika na kumshilika mama huyo, mtoto huyo alikimbizwa katika hospitali ya Malda Medical center huku akiwekwa katika chumba cha uangalizi maalum kutokana na kuwa na majeraha makubwa.Polisi walisema pamoja na mama huyo kudaiwa kuwa na matatizo ya akili pia pombe pamoja na madawa vimechangia yeye kufanya tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post