Picha zaidi ya 30!!MAZISHI YA MWANDISHI WA HABARI EDSON KAMUKARA,KIFO CHAKE UTATA MTUPU..,WENGINE WADAI KAUAWA NA VIGOGO




Mwili wa mwandishi wa habari Edson Kamukara umezikwa jana Juni 29,2015 katika kitongoji cha Bukujungu,Ihangiro wilayani Muleba,huku wale waliopata nafasi ya kutoa salamu za rambi rambi wakiweka wazi kuwa chanzo cha kifo chake bado ni utata na kwamba kimetokana na kazi yake ya uandishi wa habari.

Akizungumza katika maziko hayo, mkurugenzi wa kampuni ya mwana halisi publishers LTD Bwana Said Kubenea, alisema kifo cha marehemu Kamukara, kimezua utata kutokana na hakuna anayejua undani.


Alisema kuwa madakatari wanasema inaonekana alikufa baada ya kukosa hewa huku, chumbani kwake kukikutwa na damu, huku akiongeza kuwa
Edson alikuwa anakamilisha kazi ya uandishi uliokuwa ukiwahusu vigogo na kama habari zake zingetoka, saivi nchi ingekuwa inaongea mambo mengine.

Edson Slavatory Kamukara, amezikwa kijijini kwao Ihangiro wilayaniMuleba, huku akiacha majonzi kwa familia yake, baada ya kuacha mtoto mmoja ilhali mama yake akisumbuliwa na kupooza, ambapo siku chache zilizopita, Edson alitokea Muleba kumuangalia mama yake, kama alivyozungumza dada wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Joyce.

Marehemu Edson Kamukara, ameacha mtoto anakadiriwa kuwa na miaka kati ya 3 hadi 4 aitwaye Edgar Ishengoma, na marehemu alianza kazi ya uandishi katika gazeti la Majira, akafanya Jambo leo, Tanzania daima, na hatimaye mwanahalisi publishers ambapo amefanyia kwa kipindi cha miezi minne, na alikuwa anakamilisha habari kuhusu matatizo ya wananchi kupitia viongozi mkoani Kagera.

ANGALIPA PICHA HAPA CHINI KUTOKA KIJIJINI ALIKOZIKWA


Mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Salvatory Kamukara aliyefariki alhamisi ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam umezikwa jana Nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera katika Kijiji cha Ihangiro kitongoji cha Bukujungu na kuagwa na mamia ya waombolezaji.Marehemu Edson alizaliwa 27,03.1980 na kufariki wiki iliyopita juni 25, 2015 na amezikwa Jumatatu Juni 29, 2015. Marehemu walizaliwa Mapacha na ameacha Pacha mwenzake Edda na ameacha Mtoto wake anayeitwa Edgar.
Viongozi Dini wakiongoza ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu.
Pacha wa Marehemu Edson(kushoto) Dada Edda na Kulia ni Dada yao Jeniffer kwenye masikitiko makubwa ya Kuondokewa na Ndugu yao.Katikati ni Dada Joyce akiwa na baadhi ya Wanafamilia.Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea(kulia) akifafanua jambo na Bw. Ansbert Ngurumo aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima,Sasa ni mgombea Ubunge Muleba Kaskazini kupitia CHADEMA.
Sehemu ya Wanakwaya wakiendelea kuimba nyimboPacha wa Marehemu(kushoto) kwa machungu akiangalia Picha ya Ndugu yake wakati wa Kumuaga kuelekea nyumba yake ya Milele Juni 29, 2015. Viongozi wa Dini wakitoa salaam zao za mwisho
Pacha wa Marehemu akimuaga kwa kutoa salaam zake za mwisho!.
Dada wa marehemu Edson Salvatory Kamukara akitoa heshima za mwisho leo jumatatu jioni wakati wa kumuaga.



Heshima za Mwisho,Pacha wa marehemu na mtoto wa Kamukara.Kulia ni Mkurugenzi wa Radio Kasibante Fm 88.5 nae alikuwepo na hapa akitoa salaam zake za mwisho.

Dada yake mkubwa na marehemu Joyce akisoma kwa ufupi historia ya Marehemu Mdogo wake Edson Salvatory Kamukara,
Mwandishi wa TBC Charles Mwebeya akitoa neno.

Mwandishi mkongwe Bw. Ansbert Ngurumo akitoa neno kuhusu msiba huo wa Mhariri Marehemu Edson S. Kamukara leo wakati wa Kumuaga rasmi Kijijini kwao Ihangiro Muleba.

Umati mkubwa wa Watu walijitokeza kumuaga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea akitoa neno kuhusu kifo cha Kamukara.Ameahidi kampuni ya Mwanahalisi Publishers alikokuwa akifanya kazi kuwa itamsaidia mtoto aliyeachwa na Kamukara. Mwandishi wa TBC Charles Mwebeya akitoa neno kwa Niaba ya waandishi wa Habari Kagera waliojumuika pamoja katika sehemu hiyo kuuaga mwili wa mwenzao Edson Salvatory Kamukara,
Wakati huo huo Mama Mzazi wa Marehemu Edson hakuweza kushiriki alibaki ndani chumbani kwa sababu ya Ugonjwa alionao/ Mlemavu wa Viungo.
Waandishi wa habari Kagera wamejumuika Kuubeba mwili wa Marehemu Edson kuelekea kaburini.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka mkoani Kagera na Dar es salaam wakiwa wamebeba Mwili wa Edson kuelekea kaburini.Pacha wa Marehemu akisikitika kuondokewa na mwenzie waliozaliwa pamoja.Dada wa marehemu Edson akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Salvatory Kamukara.

Edda Pacha wa Marehemu akiwa kwenye huzuni kubwa
PICHA ZOTE KWA HISANI YA .www.harakatinews.co.tz

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527