News Alert_MSANII BEN POL ANUSURIKA KUFA KWENYE BOTI

SEA 

Mwimbaji Ben Pol staa wa hit single ya ‘Sophia’ amenusurika kifo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria na wenzake kuzimika katikati ya safari.

Baada ya kunusurika na baadae kuokolewa, Ben aliandika maneno yafuatayo kwa herufi kubwa >>> ‘MUNGU MKUBWA NA NINAMSHUKURU SANA KWA KUNIPA NAFASI NYINGINE YA KUISHI DUNIANI, We had a very bad experience today, Tumekaa ndani ya maji kwa zaidi ya lisaa, in the middle of nowhere, baada ya boat tuliyopanda kuingia maji na engine kuzimika, maji yalizidi kujaa , Boat ikazama

Cha kushukuru mungu wengi tulivaa life jackets, na baada ya kukaa majini kwa zaidi ya lisaa ilipita boat ya Wavuvi Wakatuona, Ila kati ya wote tuliyokuwepo kuna mtu mmoja hatujui alipo, na hakuwepo kati ya watu tuliyookolewa, Hawa unaowaona hapa ndio tuliopona, Wanawake watatu, watoto hao walikuwa watatu, wanaume tulikuwa nane, lakini mmoja ndiye hatujui alipo’
Ben Pol kuzama
Hii ni picha aliyoiambatanisha Ben Pol baada ya kuandika hayo maneno kwenye Instagram.

Chanzo-Millardayo.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post