Kali ya Mwezi wa Ramadhani!! BINTI ALIYEGOMA KUFUNGA ANASWA AKIFANYA UJINGA NA WANAUME WAWILI GHETONi ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani! Katika hali ya kushangaza, binti aliyejitambulisha kuwa ni mtoto wa Mzee Abass (20), mkazi wa jijini Tanga anadaiwa kugoma kufunga kisha kutoroka kwao na kunaswa geto na wanaume wawili mkoani Tanga.


Sekeseke hilo lililofunga mtaa na kujazaa umati lilijiri Ijumaa iliyopita, majira ya saa 1:00 asubuhi kwenye Mtaa wa Mbago-Manzese Kata ya Mafiga mkoani Tanga ambapo baba mdogo wa binti huyo alitoa taarifa kwa kamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na Jeshi la Polisi ambao waliingilia kati na kuvamia geto hilo.


Polisi wakiwa wamemuweka binti huyo chini ya ulinzi.


Polisi walipoingia kwenye geto hilo walimkuta binti huyo na mmoja wa wanaume hao ambaye alijitambulisha kwa jina moja Rajabu.Wakati polisi wakitekeleza majukumu yao waliushirikisha uongozi wa serikali ya mtaa huo.Hata hivyo, kufumba na kufumbua mwanaume aliyekutwa na binti huyo alipata upenyo akatimua mbio na kumwachia msala binti huyo.


Mbele ya mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Amiri Bawaziri, binti huyo alikiri kutoroka kwa wazazi wake Tanga na kwenda kuishi na jamaa huyo ambapo kwenye geto hilo pia kuna mwanaume mwingine ambaye huwa wanalala watatu kitanda kimoja.Kwa mujibu wa baba mdogo wa binti huyo, msichana huyo amemaliza kidato cha nne ambapo wazazi walikuwa wakimtafutia chuo.


Polisi wakijiandaa kuondoka naye kwa ajili ya hatua nyingine.


Alipotakiwa kuelezea namna walivyogundua kuwepo kwenye geto hilo baba mdogo huyo alisema:


“Tulimtafuta rafiki yake ambaye baada ya kumbana alisema binti yetu yupo hapa Morogoro na amekuwa akiwasiliana naye kupita simu ya huyo mwanaume wake ambaye walifahamiana kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.….majirani na mashuhuda wakitoa maelezo au kuelezea juu ya tukio hilo.


“Baada ya kuwasiliana na namba hiyo, tulitumia mbinu za kumdanganya mwanaume huyo hadi tukapajua kwenye geto lao kweli na tumefanikiwa kumpata.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post