Taharuki !! MAREHEMU AFUFUKA AKIOSHWA ILI AVISHWE SANDA,WAOSHAJI WATIMUA MBIO




Huko mjini Bagamoyo katika eneo lijukanalo kwa jina la Majani Mapana kumetokea taharuki kubwa baada ya habari kuenea kuwa kuna 
mwanamama aliyetambulika kwa jina moja la Bi. Hatujuani aliyethibitishwa kuwa umauti umekuta, kafufuka baada ya kuthibitishwa na madaktari kuwa amefariki.


Bi. Hatujuani aliugua kwa muda na kukimbizwa hospitali ya wilaya Bagamoyo na baadaye kudhaniwa kuwa ama amepatwa na umauti baada ya kuugua malaria lakini hospitalini hapo walithibitisha kuwa ameshafariki dunia. 


Mkasa huo ulitokea tarehe 28 Juni 2015 na wanandugu walishachukua maiti na matayarisho ya maziko yakiwa mbioni, turubai lilishafungwa,sanda tayari hadi Juni 29, 2015 wakimuosha maiti Bi. Hatujuani mwenye umri wa miaka 30, waliokuwa wakimuosha walishtuka maiti kuwa ana joto kali, anatoka jasho na anakunja na kukunjua mikono na miguu, lakini kusema wala kusimama hawezi wakaamua kutimua mbio!


Baada ya wanandugu kutangazia umma kuwa msiba hakuna tena bali tuna mgonjwa mahututi, waliofika msibani na umati wa watu waligoma kuondoka mazikoni hadi kieleweke nini kilichozua mtihani huu tena katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.


Timu ya Malunde1 blog ilifunga safari hadi Bagamoyo na kukuta umati wa watu katika nyumba ambayo marehemu alikua akiishi ikiwa ni muda mchache baada ya mwili wake kurejea kutoka hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo ndipo alipofariki.

Majirani walidai baada ya mwili wa marehemu huyo kurudishwa nyumbani ili kuanza taratibu za mazishi walishangaa kuona bado mwili wa moto na alikuwa akijitingisha wakati waoshaji wakimuandaa kwa ajili ya kumzika.

Majirani hao walisema waoshaji waliamua kutimua mbio baada ya kuona marehemu bado wa moto na kuzua taharuki hiyo iliyowaacha watu wengi midomo wazi.
Shangazi wa marehemu alisema ni kweli baada ya kumleta walishangaa mwili ukiwa wa moto na mapigo ya moyo yakifanya kazi kama kawaida licha ya madaktari kuthibitisha kuwa amefariki, na wakaamua kusimamisha shughuli za mazishi hadi kesho yake walipoona  amekuwa wa baridi na tayari alishafariki.

Daktari aliyethibitisha kama marehemu amefariki alisema baada ya kumpima marehemu alikuwa amefariki na kuruhusu taratibu ziendelee, na alisema kuwa mwili wa marehemu kuwa wa moto inategemee na mazingira ya sehemu alipohifadhiwa.

Baada ya madaktari kuthibitisha kwa mara ya pili kuwa bi Hatujuani kafariki,taratibu za mazishi ziliendelea..

  Na Mwandishi maalum wa Malunde1 blog- Bagamoyo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527