WAKAZI WILAYA YA KAKONKO WATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF-KIGOMA

Katibu tawala wilaya ya Kakonko Bi.Zainab Mbunda akifungua Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Afya ya Jamii CHF uliofanyika katika Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko huo wa hiari ambao unawawezesha kupata huduma za matibabu kwa muda wa mwaka mzima baada ya kujiunga na kuchangia kiasi cha shilingi elfu kumi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko Bi.Jaina Msangi akizungumza namna ambavyo Halmashauri inavyosimamia Mfuko huo wa CHF na kueleza kuwa wamekuwa wakihamasisha Jamii kujiunga na Mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma za Afya.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw.Rehan Athuman akitoa maelezo mafupi kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii CHF na namna ambavyo ulivyoweza kuwafikia watanzania na kunufaika na huduma za Mfuko huo unaolenga kuboresha afya za wananchi hususani wenye kipato cha chini na cha kati.
Baadhi ya Wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya waliohudhuria katika Mkutano huo wakiwemo Madiwani,Watendaji wa vijiji,Kata na Vitongoji,Viongozi wa Dini,Vyama vya Siasa,Mashirika,Asasi mbalimbali na Wazee Maarufu wa wilaya ya Kakonko(Picha zote na  KAPIPIJhabari.COM) 






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post