LOWASA AKUSANYA MILIONI 200 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE YA KIISLAM HUKO ARUSHA



Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasili jijini Arusha kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akilakiwa na baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu jijini Arusha alipowasili kwa ajili ya kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi.
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowasa ameendesha harambee na kuchangisha zaidi ya milion mia mbili kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kiislam inayojengwa mkoani Arusha.

Katika harambee hiyo Lowasa ambaye alipata mapokezi makubwa kutoka kwa wananchi na viongozi wa mkoa wa Arusha aliwasilisha mchango wa milioni mia moja na tano zilizojumuisha mchango wake mwenyewe na wadau wadau mbali mbali akiwemo makamu wa rais Dr. Mohamed Gharib Bilal aliyemwakilisha.

Akizungumza katika harambee hiyo Sheikh mkuu wa mkoa wa Arusha Shaban Bin Jumaa pamoja na kuwashukuru wote waliojitolea  amewataka watanzania kuendelea kuonyesha umoja wao kwa vitendo kwa kusaidiana bila kuongiza itikadi zao za kidini na za kisiasa.

Katibu wa Bakwata mkoa wa Arusha Bw Abdalah Masoud amesema shule hiyo ya sekondari ya kiislam inayojengwa katika eneo la Tengeru   wilayani Arumeru inatarajiwa kugharimu zaidi ya bilioni moja itakapokamilika na itasomesha watoto wote bila kujali itikadi zao.

Harambee hiyo ilihudhuriwa na wananchi na viongozi wa kada mbalimbali, wakiwemo wa kisiasa, wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wa madini, na vijana wanaoendesha pikipiki maarufu kama bodaboda.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post