Ajali!! BASI LA WANAFUNZI LAGONGANA LORI LA MCHANGA!!,ANGALIA PICHA HAPA


Haice ilivyokuwa ikionekana muda mfupi baada ya ajali
Lori la mchana likiwa limepinduka baada ya ajaliAjali hiyo  imetokea leo jioni   eneo la Boma mbuzi pasua katika barabara iendayo kiwanda cha sukari TPC,imehusisha magari mawili ambayo ni Toyota haice yenye namba za usajili SU 37299 mali ya chuo cha mafunzo ya ufundi VETA lililogongana uso kwa uso na Tipa la mchanga lenye namba za usajili T 202 BFT na kusababisha tipa hilo kupinduka.
Kwa mujibu wa maelezo ya askari wa barabarani aliyefika katika eneo la tukio,aliyepata majeraha makubwa ni dereva (mwanafunzi) ambaye jina lake halijafahamika na amewahishwa kupata matibabu.Kwa upande wa dereva wa lori hilo bwana Victor ambaye amepata mshituko katika mguu wake wa kulia ameelezea chanzo cha ajali hiyo kuwa ni dereva wa haice kuingia kwa kasi katika barabara hiyo akitokea upande wa kushoto wa barabara hiyo hivyo na kushindwa kulimudu gari na hatimaye kulifuata lori hilo.
Kushoto ni dereva wa Lori akiongea na askari wa barabarani ,aliyejishika kifuani ni mwalimu wa VETA aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi katika haice iliyohusika katika ajali

Utingo wa lori akikusanya mchanga uliomwagika baada ya ajali
“Mimi nilikuwa nikipandisha kutokea upande wa Serengeti (breweries)   kwa kawaida nilitegemea derevawa haice angesubiri nipite kwani nilikuwa upande wake wa kulia lakini cha kushangaza aliingia bila kutoa ishara na gari ilipomshinda alikuja upande wangu,nilijaribu kumkwepa lakini ilishindikana kwani alisha karibia sana na baada ya kugongana gari langu lipinduka kutokana na uzito wa mchanga niliyokuwa nimebeba”.
Askari wa barabarani akijaribu kuwatuliza wananchi walitaka kumpiga mwalimu wa VETA
Hali ya tafrani ilizuka mara baada ya mwalimu wa VETA kumueleza askari wa usalama wa barabarani waliofika eneo hilo kuwa yeye pamoja na wanafunzi wake walikuwa wakitokea upande wa mjini jambo lililopingwa vikali na mashuhuda wa ajali hiyo kitendo kilichopelekea askari kuwatuliza wananchi hao ambao walitaka kumpiga mwalimu huyo.

Akizungumza na mwandishi wetu huku akiwa haoneshi ushirikiano wa kutosha mwalimu aliyekuwa akiwasimamia wanafunzi hao wa VETA (hakutaja jina) alieleza kuwa ndani ya haice kulikuwemo na wanafunzi ishirini akiwemo aliyejeruhiwa(dereva).
Askari wa barabarani wakifanya vipimo katika  ajali 

“Huyu mwalimu ndiyo mwenye makosa ,huwezi kumruhusu mwanafunzi aingize gari barabarani katika hali kama ile” alieleza bwana Hamis Mbwana mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.
Wananchi waliokuwa wakishuhudia matukio yaliyojiri eneo la tukio

Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio gari maalum kwa ajili ya kuvuta na kuondoa magari hayo lilifika  ili kuruhusu shughuli nyingine za matumizi ya barabara kuendelea.


  Habari,Picha Na Dickson Mulashani

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post