Wakati Albino Wakizichapa Ikulu DAR ,HUKO GEITA WATU WANNE WALIOUA ALBINO WAHUKUMIWA KUNYONGWA!!



Mahakama kuu ya Tanzania katika kikao chake kilichofanyika mkoani Geita imewatia hatiani na kuwahukumu kunyogwa mpaka kufa, watuhumiwa wa nne wa mauaji ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi Zawadi Magindu aliyeuwawa mwaka 2008 katika kijiji cha Nyamalulu wilayani.

Awali akisoma shitaka hilo mbele ya jaji wa Joacqune Mello mwanasheria wa Serikali Eziloni Mwasimba aliambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 11.03 .2008 majira ya saa moja jioni washitakiwa  4 ambao ni Masalu Kahindi, Ndalanya Rumora, Singu Siantemi, na Nasoro Saidi, huko katika kijiji Nyamalulu Wilayani Geita walimuua kwa kumkata mapanga na kusababishia kifo kilichotokana na  kuvuja damu nyingi.
 
Eziloni aliongeza kuwa watuhumiwa hao baada ya kutenda unyama huwa walikimbilia sehemu mbalimbali za vijiji vingine  ili wasikamatwe na mkono wa sheria hivyo akiomba Mahakama kutoa hukumu kali dhidi ya watuhumiwa ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye nia kama hiyo.

Mara baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote bila kuacha shaka lolote ndipo mahakama hiyo kwa kutumia kifungu cha sheria 196 na 197 ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
 
Kwa mujibu wa mashahidi waliojitokeza inasemekana mtuhumiwa namba mbili Ndahanya Lumola na mtuhiwa namba tatu Singu Siantemi ndio waliohusika na upimaji wa mifupa ya marehemu Zawadi ambapo hutumia wembe na shilingi moja kuweka karibu na mifupa ya Albino ili kujua kama itavuta kama sumaku na kipimo kingine ni redio ambayo huiweka karibu na mifupa na ikizimika ndio mifupa hiyo huonekana kuwa na ubora tofauti na hapo mifupa hiyo huwa haifai na hutupwa.
 
Mashahidi hao wamesema vipimo hivyo havina uhalisia wa aina yoyote kwani hakuna binadamu mwenye mifupa inayokuwa na sumaku.
 
Kwa kuzingatia ushahidi na utetezi wa pande zote jaji Joaquine De-mello amesema mahakama imejiridhisha pasipo kuacha shaka yoyote kuwa watuhumiwa wote wanne walihusika na mauaji ya Bi Zawadi Magindu katika kijiji cha Nyamalulu wilayani Geita mnamo tarehe 11 mwezi wa tatu mwaka 2008 usiku.
  
Aidha jaji De-mello amesema anashangazwa na kesi zote alizosimamia zinazohusu mauaji ya Albino watuhumiwa wote wanaofikishwa mahakamani ni wakataji wa mapanga na kuhoji wakataji hao wanapeleka wapi mifupa hiyo? Na kuwataka wahusika kuhakikisha wanawapata wanunuzi na watumiaji wa viongo hivyo vya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Hata hivyo baada ya hukumu hiyo kutolewa baadhi ya wananchi waliokuwa mahakamani akiwemo mwenyekiti wa walemavu wa ngozi mkoa wa Geita na wengine wenye ulemavu mbali na kuipongeza mahakama kwa kutoa hukumu ya haki inayoashiria kuwapa ulinzi jamii hiyo ya maalbino pia wamesema mahakama haikutenda haki kwani kuna watuhumiwa wengi walitajwa kwenye kesi hiyo lakini hawakuonekana mahakamani.

Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post