MWANAFUNZI APOOZA MWILI WOTE BAADA YA KULA CHOCOLATE ALIYOPEWA NA MARAFIKI ZAKE

IMG_1619_2 

Mwanafunzi mmoja ambaye umri wake ni miaka 17 Marekani amelazwa baada ya kupata ugonjwa wa kupooza baada ya kula chocolate aliyonunuliwa na marafiki zake ambao wanasoma darasa moja katika shule ya Benjamin Banneker High School huko Brooklyn.

Mwanafunzi huyo Danieel Buchanan aliletewa chocolate na wanafunzi wenzake ambavyo walikula wote, muda mfupi baadae hali ilikuwa mbaya akapelekwa Hospitali ambapo muda mfupi baadae mtoto huyo aliruhusiwa kuondoka na wazazi wake.

Muda mfupi baadaye hali ya Buchanan ilibadilika tena, akashindwa kuongea, kutembea, kula na miguu yake kupooza.. 

Mama yake akaamua siku ya pili yake kumpeleka Hospitali ya Mount Sinai ambapo baada ya kufanyiwa vipimo ilionekana kuwa kwenye chocolate aliyokula kulikuwa na bangi, rafiki ambaye alimpa Buchanan chocolate hiyo alisimamishwa shule anayosoma huku Polisi wakiendelea na upelelezi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527