Kumekucha NIGERIA !!! WAPINZANI WABEBA NCHI!!,BUHARI AMBWAGA VIBAYA RAIS GOODLUCK JONATHAN



Rais mpya wa Nigeria Buhari
Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Nigeria kaskazini.
Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.
Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi katika Nigeria, Uingereza, India, na Marekani.
Na aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa Mfuko wa Amana ya Mafuta.
Wafuasi wa rais Buhari wakishangilia ushindi huo
Anasemekana kuwa si m-kaishi, hakubali kushindwa.
Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,
Mkristo, anaye toka eneo la Niger Delta, kusini Nigeria, kwa mara ya pili, katika uchaguzi wa Machi. Unaonesha kuwa mchuano mkali.
Kuambatana na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni. Kushindwa mwaka 2003 na tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani bila mafanikio.
Buhari alimshinda rais anayeondoka Goodluck Jonathan katika uchaguzi ulioshuhudia ushindani mkubwa
Ingawaje, Buhari anazingatiwa kuwa kiongozi mwenye ufuasi mkubwa na heshima nyumbani, hususan katika rubaa za kaskazini Nigeria.
Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi.

map showing who has won each state
Kimataifa, Buhari pia anasemekana kuheshimiwa.
Yajulikana kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu ndio Wafrika binafsi waloalikwa na Ikulu ya White House, Marekani, kuhudhuria sherehe za kutawazwa Barack Obama.
Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,
umeme na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake, usalama, na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?.
&&&&&&&&&&


Jenerali Muhammadu Buhari alikuwa anaongoza kwa zaidi ya kura milioni mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye ni rais Goodluck Jonathan 

Kura zilizopigwa siku ya Jumamosi huko Nigeria.

Generali Buhari wa chama cha All Progressives Congress (APC) alionekana kusajili matokeo mema mapema hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini Lagos.
 
 Mgombea wa upinzani Muhammadu Buhari amekuwa mbele ya rais wa sasa Goodluck Jonathan.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527