Picha>>KIFO CHA ABDUL BONGE WA TIP TOP CONNECTION UTATA MTUPU,ANAYEDAIWA KUHUSIKA KATIKA MAUAJI ATOROKA

 
Umati wa vijana ukiwa hauamini kutokea kwa kifo cha Abdul Bonge.
 
Meneja wa TMK Wanaume Family, Yamoto Band na Diamond, Said Fella akiwaeleza kinachoendelea baadhi ya mastaa waliofika msibani hapo.
 
Msanii wa filamu za Kibongo, Baba Haji, akiwaelekeza wenzake ulipo msiba.
 
Mdogo wa marehemu Abdul Bonge, Bab Tale akihojiwa na Mwandishi Mwandamizi na Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Global Publishers, Richard Bukos.
 
Fella akiwaeleza jambo vijana wake.
 
Waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni msibani hapo.
 
Mdogo wa marehemu, Habib Uledi (kushoto) akimueleza jambo msanii wa filamu za Kibongo, William Mtitu.
 
Wasanii wa filamu za Kibongo, Baba Haji na Riyama Ally wakisalimiana kwa kimtindo.
 
Mchekeshaji Kitale a.k.a ‘Mkude Simba’ akiingia msibani huku akifuatiwa na mchekeshaji mwenzake, Stan Bakora.
 
Wasanii wa filamu za Kibongo wakisalimiana.
 
Mdogo wa marehemu aitwaye Idd ambaye alikuwa ndiye wa kwanza kuitwa baada ya kaka yake kuanguka.
 
Kitale na Baba Haji wakifurahia jambo baada ya kukutana.

@@@@@@
KIFO cha mdau wa muziki nchini ambaye ni mwanzilishi na meneja wa kundi la Tip Top Connection, Abdul  Shaban Taletale, kilichotokea Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam, jana jioni kimeendelea kuzua utata kufuatia mtuhumiwa wa mauaji mtu aliyetajwa kwa jina la Nassoro Idd kuingia mitini. 

Akizungumza na mandao huu, Meneja wa Kundi la Tip Top Connection na mdogo wa marehemu, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’, alisema siku ya tukio Abdul Bonge akiwa maskani ya Tip Top Connection iliyopo Magomeni-Kagera alifuatwa na kijana mmoja na kuambiwa rafiki yake aitwaye Nassoro Idd alikuwa akipigana na mkewe hivyo aliagizwa na mama yake Nassoro akamwite ili awasuluhishe. 

Muda mfupi baada ya kwenda kwenye ugomvi huo zilirudi taarifa kuwa Abdul Bonge ameanguka na kupoteza fahamu.
Bab Tale alisema walimpeleka Hospitali ya Saint Monica iliyopo Manzese-Darajani lakini waliambiwa tayari ndugu yao alikuwa amepoteza maisha. Kufuatia tukio hilo Nassoro ametorokea kusikojulikana lakini mkewe anashikiliwa na jeshi la polisi. 

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa muda wowote kwenda Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro baada ya polisi kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo na kuwakabidhi mwili huo.
(PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527