Ishu ya imani ni ya mtu binafsi na kila mtu ana uwezo wa kuamini kile anachoona ni sahihi kwa mtazamo wake na mtu anapotokea kumuamini kiongozi wake wa dini kwa asilimia kubwa hutekeleza yale anayofundishwa.
Sasa hii ya leo inamuhusu mhubiri maarufu wa dini India ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni hamsini duniani Gurmeet Ram Rahim Singh
anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha majeruhi kwa tuhuma za
kuwashawishi wafuasi wake 400 kukata sehemu zao za siri ili waweze kuwa
karibu na Mungu.
Mmoja wa wafuasi wake, Hans Raj Chauhan
aliwaambia Polisi kwamba alikatwa sehemu zake za siri kwa sababu
alidhani asingetakiwa kwenye jamii kama angekataa kutekeleza utaratibu
huo ulioanzishwa Singh.
Singh aliwaambia wafuasi wake kwamba wale ambao wanaotekeleza amri hiyo watakuwa na uwezo wa kumuona Mungu.


Social Plugin