BASI LAGONGANA NA HIACE ENEO LA KITULI SHINYANGA,DEREVA WA HIACE NA ABIRIA WAFARIKI


Gari ndogo iliyosababisha ajali ikiwa eneo la tukio-Picha na Richard Kabega-Malunde1 blog Shinyanga

Basi la Mantale Tours likiwa eneo la tukio-Picha na Richard Kabega-Malunde1 blog Shinyanga



Watu wawili wanadaiwa kufariki dunia katika ajali iliyohusisha gari dogo aina ya Noah na basi la Mantale Tours likitoka Mwanza kwenda Kahama katika eneo la Kituli barabara ya Tinde Kahama mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo imetokea jana saa tatu usiku ikihusisha basi hilo linalofanya safari zake Mwanza Kahama na gari hiyo ndogo inayofanya safari zake Didia hadi Shinyanga mjini.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiypo Robert Njile Monday ameiambia Malunde1 blog kuwa dereva wa gari ndogo anayejulikana kwa jina la  Chomola  aliyefariki papo hapo alikuwa katika mwendokasi na kusababisha ajali hiyo.

Amesema kutokana na mwendokasi huo aligonga bams iliyopo katika eneo la barabara ya kwenda Shule ya sekondarii Kituli gari ikamshinda na hatimaye kugongana na basi hilo.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa gari ndogo ilikuwa na dereva na abiri mmoja anayedaiwa kufariki pia ambapo dereva wa basi aliumia kidogo na abiria wake

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post