MWANAJESHI WA JWTZ AUA MTOTO WA ASKARI POLISI MJINI SHINYANGA

Image result for KAMANDA KAMUGISHA
Askari wa jeshi la wananchi (JWTZ) Ng’habi Mayenzi (48), kikosi cha kambi ya Kizumbi 516 KJ, Shinyanga amesababisha kifo cha mtoto wa askari polisi papo hapo Ester Daudi(05) baada ya kumgonga na pikipiki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kwa vyombo vya habari Justus Kamugisha ,alisema tukio hilo limetokea Machi 26 mwaka huu,majira ya saa saa saba mchana katika eneo la kanisa la Wasabato barabara ya stendi ya mjini Shinyanga kuelekea Kambarage.

Alisema pikipiki iliyosababisha kifo cha mtoto Ester Daudi (05), ambaye pia ni mwanafunzi wa chekechea na mkazi wa kambi ya jeshi la Polisi kata ya Kambarage ni yenye namba za usajili MC 411 ADB aina ya Kinlion.

Alisema mtoto aliyegongwa ni mtoto wa askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga CPL Daudi.

Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi aliokuwa nao mwanajeshi Ng’habi Mayenzi, ambapo baada ya kumgonga mtoto huyo na kusababisha kifo chake naye alikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kutokana na kuumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake.

Aidha Kamugisha alisema,kutokana na majeraha aliyokuwa nayo mwanajeshi huyo, hali ilizidi kuwa mbaya na ilipofika  Machi 27, majira ya saa moja asubuhi  alifariki dunia.

Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527