ANGALIA PICHA- MAGARI HAYA LEO YAMEKABIDHIWA KWA AJILI YA USAFI KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA
Monday, March 16, 2015
Hapa ni ofisi za halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ambapo
leo Jumatatu Machi 16,2015,Kampuni ya uuzaji magari na mitambo nchini Tanzania
GF Trucks and Equipment Limited yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam imekabidhi
magari mawili (Tipper)(PICHANI) kwa halmashauri hiyo yenye thamani ya shilingi milioni
235 yatakayotumika kwa ajili ya usafi katika mji wa Shinyanga pesa zilizotolewa
na benki ya dunia kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali katika halmashauri-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Mhandisi mwandamizi idara ya Mauzo na Masoko
kutoka Kampuni ya uuzaji magari na mitambo nchini Tanzania GF Trucks &
Equipment Limited Juma Hamsini( mwenye shati jeupe kushoto) akikabidhi ufunguo wa
gari kwa meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamhafeez Abubakar Mukadam( katika
ofisi za manispaa hiyo.Tukio hilo limeshuhudiwa na madiwani wa manispaa hiyo
Picha ya pamoja wakati wa makabidhiano hayo,wa kwanza kushoto ni Mhandisi mwandamizi idara ya Mauzo na Masoko
kutoka Kampuni ya uuzaji magari na mitambo nchini Tanzania GF Trucks &
Equipment Limited Juma Hamsini,akifuatiwa na meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamhafeez Abubakar Mukadam,wa kwanza kulia ni mratibu wa mradi wa benki ya benki ya dunia(Focal Person) manispaa ya Shinyanga Mwambuli Mwasaga,akifuatiwa na mratibu wa mradi huo Injinia Simon Ngagani
Diwani wa CHADEMA kata ya Kambarage bwana Nyangaka Shilungushela akiwa ameshikilia ufunguo. Wiki
hii pia kampuni hiyo itakabidhi katapila (greda) moja lenye thamani ya shilingimilioni 520 kwa ajili ya ujenzi wa barabara
mbalimbali katika mji wa Shinyanga.
Social Plugin