Picha Zinatisha!! JAMAA AMUUA MKE WAKE KWA KUMTOBOA KIFUA WAKIWA GESTI

Mwili wa marehemu
Mtuhumiwa wa mauaji
 Mkazi wa Tabata Mawenzi, Remi Joseph (36) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumkata kichwa kwenye nyumba ya wageni ya Friends Corner ya jijini Dar es Salaam.


Aliyeuawa ni Josephena Moshi (35), ambaye alikatwa kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani wakiwa kwenye nyumba ya wageni ya Friends Corner.



Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa  Kinondoni, Augustine Senga, alikiri kutokea mauaji hayo.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi saa 8:00 mchana na kwamba familia hiyo ilikuwa inaishi Tabata Mawenzi.

Senga alisema mwanamke huyo alifariki papo hapo baada ya kushambuliwa na kwamba chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika na uchunguzi unaendelea.

Kamanda Senga alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi.



Hata hivyo, gazeti hili lilijulishwa kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kufanya mauaji hayo, alifanya jaribio la kutaka kujiua lililoshindikana.


Kamanda alipoulizwa kuhusiana na mtuhumiwa huyo kutaka kujiua, alisema kuwa uchunguzi unaendelea.


“Bado ni mapema sana kueleza kila kitu hayo niliyokueleza ni taarifa za awali kwani na huyu mtuhumiwa amekutwa na majeraha shingoni, hivyo masuala ya kazi yake na sababu vinachunguzwa,” alisema Senga.

 Na Beatrice Shayo-Dar es salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post