Noma Kweli! MAMA MCHUNGAJI AFIKISHWA MAHAKAMANI KISA KUSUMBUA WATU KWA KUHUBIRI KWA SAUTI KUBWA MTAANI

prayer26n-1-web
Mama Mchungaji, Martha Nagbe


Martha Nagbe alijikuta akitozwa faini na Mahakama kwa kesi ya usumbufu na kupigia kelele majirani na wapita njia, lakini ukweli ni kwamba alipigwa faini hiyo kutokana na kufanya mahubiri barabarani kwa sauti ya juu na sio kwamba alikuwa akipiga kelele.

Mke huyo wa mchungaji ambaye amekutana na mkasa huo Dakota, Marekani amepigwa faini hiyo baada ya kukutwa mara kadhaa akihubiri barabarani jirani na makazi ya watu ambao nao waliwahi kulalamika kwamba wanakerwa na kelele za mama huyo, mwisho wa siku Polisi wa doria walimkuta na kumpeleka Mahakamani ambako alipigwa faini ya dola 150 ambazo ni zaidi ya 270,000/- Tshs.
prayer26n-3-web
Mchungaji Juwle Nagbe
Mume wa mwanamke huyo Mchungaji Juwle Nagbe amesema mke wake amesikitishwa sana na maamuzi ya Mahakama hiyo na anauona kama ni uonevu.
Kanisa I
Kanisa la Methodist lililopo Lisbon, Dakota Kaskazini, Marekani ambalo mume wa Martha ni Mchungaji wa kanisa hilo

Mbali na kupigwa faini hiyo Martha amesema hatoacha kusali kwa sababu ana imani na MUNGU na pia anaamini yuko huru kuendelea kufanya mahubiri kwa njia yoyote ambayo ataona iko sawa na imani yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527