TAARIFA KUHUSU BINTI ALIYEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA KATIKA KATA YA SOLWA SHINYANGA VIJIJINI

Pichani ni binti huyo akiwa ameuawa na watu wasiojulikana
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Huma Simon (27) mkazi wa kitongoji cha Solwa Kata ya Solwa Wilayani Shinyanga Vijijini ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia siku ya Alhamis Februari 19,2015.

Kwa mujibu wa Majirani Mwili wa marehemu Huma umekutwa asubuhi katika eneo la Shule ya msingi Solwa ukiwa umekatwa mapanga sehemu mbalimbali na kutelekezwa.

Taarifa zimesema Huma ambaye anaishi na Mama yake Mzazi, alitoka usiku katika chumba alichokuwa amelala na kumuacha Mtoto wake wa kike anayekadiriwa kuwa na miaka miwili, na kukutwa asubuhi akiwa ameuawa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post