ANGALIA PICHA_ MAGARI YAGONGANA ENEO LA KALOGO MJINI SHINYANGA

Hapa ni katika eneo la Kalogo barabara ya Mwanza-Shinyanga ambako gari mbili ndogo ziligongana majira ya saa tatu na nusu usiku wa kuamkia leo ambapo chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa mwendo kasi wa mmoja wa madereva wa magari hayo ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo huku ndani ya gari lake kukiwa na viroba vya konyagi na bia hali ilioonesha pengine dereva alikuwa amelewa kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga


Gari inayodaiwa kuwa ilikuwa katika mwendo kasi ikiwa na watu watano na inaelezwa kuwa pia alikuwemo mtoto mchanga ambao walinusurika kufa ikiwa imepinduka
Kulia ni gari lilikuwa katika mwendo kasi likiwa limeharibika vibaya.Gari la kulia lililoharibika vibaya mashuhuda wanasema lilikuwa limebeba watu  watano huku gari jingine likiwa na dereva wake pekee,hivyo watu 6 walinusurika kufa na inaelezwa kuwa hawakupata majeraha

 Ilielezwa kuwa ndani ya gari lililoharibika kulikutwa chupa za bia na viroba vya konyagi



eneo la tukio

Gari la polisi likiwa eneo la tukio,ndani ni watu waliokuwa katika gari lililosababisha ajali

Mwonekano wa magari yote mawili

Wakazi wa Shinyana wakishirikiana na askari polisi kuondoa gari lililoharibika vibaya barabarani ili kuepusha ajali nyingine kwani mabasi ya kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza hupita hapo yakiwa katika mwendo kasi na ndipo mwaka juzi basi la Saibaba liligonga treni

Wakazi wa Shinyanga wakiwa  katika eneo la tukio,chini ni pombe ikiwa imemwagika pembeni ya gari lililokuwa katika mwendo kasi

Gari ya pili ikiwa imeharibika,ingawa dereva wake hakuumia katika ajali hiyo

Askari wa jeshi la  polisi mkoa wa Shinyanga kikosi cha usalama barabarani akimsihi dereva asiye na makosa aondoe gari barabarani baada ya kugongwa na gari iliyokuwa katika mwendo kasi na kusababisha ajali hiyo kwani aligoma kuondoa gari kwa kile kilichodaiwa kuwa gari lililogonga ni mali ya askari  polisi wa Shinyanga hivyo alitaka kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga afike eneo la tukio-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post