Wivu wa Mapenzi!! AUAWA KWA KUKATWA UUME,AKATWA KICHWA,VIUNGO VYAKE VYACHESHWA KAMA MBOGA


Mnamo 22/01/2015 majira ya 23:45hrs huko kijiji cha Songambele wilaya ya Mlele,mkoani Katavi Richard Madirisha, msukuma, 31yrs,mkulima, akiwa amelala na mke wake ghafla alivamiwa na watu wasiojulikana karibia watano ambapo walivunja mlango na kuingia ndani na kuanza kumkatakata mapanga, kutenganisha kichwa, sehemu za siri kisha kuchemsha viungo hivyo nje ambapo moto ulikuwa unawaka.

Sufuria za kuchemshia viungo hivyo walivichukua ndani ambapo walimtishia mke wa marehemu aitwaye Mekrina Moses, msukuma, 25yrs asipige kelele.

Baada ya kukamilisha zoezi walinawa mikono kwa kutumia sabuni iliyokuwa nyumbani kwa marehemu na kuondoka na simu ya marehemu yenye namba 0783846414.

Taarifa za awali inaonyesha chanzo kulipiza kisasi kwani marehemu alikuwa akiishi Kaliua mkoani Tabora na huyo mwanamke alikuwa ni mke halali wa Shija Manyama wa Kaliua hivyo marehemu alipora mke wa mtu.

Kitendo hicho kilimuudhi Shija na kuamua kukata mapanga ng'ombe 7 wa marehemu na ugomvi ukawa unaendelea hadi July 2014 ambapo marehemu alihamia kijiji cha Songambele wilaya Mlele, na hata hivyo inasemekana vitisho viliendelea kutolewa na Shija dhidi ya marehemu kwa njia ya simu.

Jitihada za kuwatafuta watuhumiwa zinaendelea. 
via>>Jamii Forums

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post